NA TIGANYA VINCENT, RS-TABORA

VIJANA wanaondesha shughuli za usafirishaji wa  abiria kwa njia ya Pikipiki (Boda boda) mkoani Tabora wamepewa jukumu la kuhakikisha wanasimamia usafi kwa kuwakamata watu wenye tabia za kutupa takataka  ovyo katika maeneo mbalimbali  miji na hivyo kuhatarisha afya za watu wengine.

Jukumu hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kanyenye wakati akiwahamasisha wananchi awamu ya pili zoezi la upandaji miti mingine na usafi wa mazingira. Alisema kuwa kuanzia sasa Boda boda watakuwa wanajukumu la kukamata watu watakaotupa taka taka za aina yoyote katika mitaa na kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi na kuwafikisha katika Halmashauri husika.

Mwanri alisema kila mtu atakayekamatwa kwa kutumia Sheria ndogo ndogo za eneo husika atalazimika kulipa silingi elfu 50 ambapo kati ya hizo mkamataji atalipwa shilingi elfu 25 zilizobaki zitakuwa mali ya Halmashauri husika.

“Ndugu zangu boda boda leo nawapa mpango mzuri wa kupata pesa ambao ni huu …ukimwano mtu katupa karatasi ya vocha kamata…ukimwona katupa gunzi kamata…chupa ya maji kamata na mpeleke Halmashauri kisha atalipa elfu 50 wewe watakupa elfu 25 mnaonaje mpango huo? Aliuza Mwanri .

Alisema kuwa haiwezekani Tabora ikaendelea kubaki nyuma katika suala la usafi na viongozi na wananchi wapo ni lazima watu wabadilike na waanze kuzingatia suala la usafi kwa ajili ya kulinda afya zao na jamii inayowazunguka. Alisema kuwa lengo la mpango huo ni kutaka kuhakikisha Mkoa mzima wa Tabora unaondokana na aibu ya kuwa na takataka zilizotupwa ovyo na hatime uwe Mkoa wa kwanza hapa nchini kwa kuzingatia usafi.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewaagiza viongozi wa Halmashauri zote kuhakikisha kuwa maduka yote yanayotoa huduma za kuuza vinywaji , vibanda vya vyakula na baa  ambazo hazina vyoo zinafungwa mara moja. Alisema kuwa hakikuta sehemu mtu anayeendesha biashara hiyo huku hana choo atalazimika kuwachukulia hatua viongozi husika ikiwemo kuwasimamisha kazi kwa kushindwa kusimamia majukumu yao ikiwemo kulinda afya za wananchi. Mwanri alisema kuwa inapotea tatizo la mlipuko wa magonjwa Serikali inaingia gharama kubwa kuhakikisha inaokoa maisha ya wananchi kwa hiyo ni vema kuchukua tahadhari mapema.

Alisema kuwa hawezi kuvumilia kuona watu wanaendelea kutoa huduma katika mazingira ambayo sio salama kwa kuwa analojukumu na dhamana ya kuhakikisha wakazi wote wa Tabora wanakuwa salama na afya bora. Mmoja wa Madreva wa Boda boda Bonos Binamungu apongeza hatua ya Mkuu wa Mkoa kuwakabidhi jukumu la kusimamia usafi na kuahidi kutekeleza jukumu hilo kwa misingi ya Sheria na taratibu bila kumwonea mtu.

Alisema kuwa kuondoa mikwaruzano ni vema wananchi wa Tabora wakaanza kutii sheria ikiwa ni pamoja na kutupa takataka katika maeneo husika ili kuepuka kupata hasara ya kulipa fedha ambazo hakutarajia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...