Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akiwa na wazazi wake katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam akisubiri kusomewa mastahaka yanaymkabili jijini Dar es Salaam leo.
 Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akiongea jambo na wakili wake, Peter Kibatala wakizungumza jambo kabla ya kuanza kusomwa kesi yake ya kuua bila kukusudia jijini Dar es Salaam leo.
Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akitoka katika mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam mara baada ya kesi yake kumaliza kusomewa na kuhairishwa mpaka Jumatatu Oktoba, 23, 2017.
Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akiwa nje ya mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa kesi ya kuua bila kukusudia ya msanii mwenzake Steven Kanumba.

Karama Kenyunko na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
DAKTARI wa familia ya msanii maarufu wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, Dkt, Paplas Kagaia, ameileza mahakama Kuu ya Tanzania kanda Dar es Salaam Kanumba alifariki toka nyumbani baada ya kumpima na kukuta mapigo yake ya moyo hayakuwepo.

Dk, Paplas amedai hayo leo Oktoba 20, 2017 huu wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Sam Rumanyika.

Amedai kuwa, baada ya mdogo wa marehemu kumfuata hospitali kwake na kumwambia kuwa Kanumba amefariki, alichukua kipino cha sukari na shindikizo la Damu(pressure) na kwenda moja moja nyumbani kwake Sinza ambako baada ya kufika nyumbani kwake alimpima sukari na kukuta io kawaida lakini alipompima pressure haikuwepo kabisa. 

Daktari Huyo mwenye elimu ya stashada ya juu (Advance diploma) aliyejipatia Elimu yake chuo cha uuguzi cha jeshi cha Lugalo amedai kuwa, alikuwa daktari wa familia ya Kanumba kwa zaidi ya miaka mitano na anamiliki Hospitali yake binafsi ya St. Anna iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam alikuwa akimtibu Kanumba magonjwa ya kawaida na hakuwahi kugundua tatizo lake lolote. 

Mahojiano kati ya Dr Paplas na Wakili wa serikali Batlida Mushi yalikuwa kama ifuatavyo;

Wakili: Ulipata wapi taarifa kama ya kuugua kwa Kanumba?
Shahidi: Nikiwa naudumia wagonjwa kama kawaida nilipigiwa simu na Seth akiniomba niende kumuona Kanumba amedondoka, nikamwambia muda ule ulikuwa ni usiku sana aende kumchukua.

Wakili: kwani nini Seth akupigie wewe simu?
Shahidi: Nilikiwa daktari wa familia yao kwa miaka kama mitano hadi sita.

Wakili: Baada ya kukupigia simu, ulifanya nini?
Shahidi: Nilichukua vifaa vya mashine ya sukari na BP, niliingia chumbani kwake nikifuatana na Seth nilipofika nilikuta Kanumba amelala chini chali, nikampima sukari ilikuwa normal nikampima pressure mapigo ya moyo hayakuwepo kabisa.

Wakili:Baada ya kujua mapigo ya moyo hayapo ulifanya ulichukua hatua gani?
Shahidi: Nilimwambia Sethi Fanya umvalishe nguo wafanye utaratibu wa kumpeleka hospitali kubwa ya Muhimbili akafanyiwe Vipimo.
Wakili: Baada ya hapo ulifanya nini?
Shahidi: Baada ya kumvalisha nguo kwa kisaidiana na kijana mmoja wa jirani na mama mwenye nyumba tulimpeleka Muhimbili kitengo cha emergency.

Wakili: Mlipofika Muhimbili kitengo cha Emergency ulifanya nini?
Shahidi: Nilimuomba Dk tuliyemkuta pale ampime Kanumba na alipompima alisema kuwa ameshafariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...