Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili katika manispaa ya Shinyanga.

Zoezi la kukabidhi sare hizo za shule limefanyika leo Alhamis Oktoba 12,2017 katika shule ya msingi Kitangiri.Msaada huo wa sare za shule unatokana na kampeni iliyoanzishwa na mkuu huyo wa wilaya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi sare hizo,Matiro alisema pamoja na serikali kuwa na sera ya elimu bure lakini wamebaini kuwa kuna watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu hivyo wanahitaji msaada kutoka wadau mbalimbali.

“Tulifanya zoezi la kugawa sare kwa wanafunzi wengine hivi karibuni,na leo ofisi yangu kwa kushirikiana na wadau wengine likiwemo shirika la wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO) nimekuja kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wa kata ya Kitangili na Kizumbi”,alieleza Matiro.Matiro aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao wa kulea watoto badala ya kuwatekeleza kwa bibi na babu zao na wao kukimbilia mjini huku watoto wakiteseka na kuishi katika maisha magumu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza kabla ya kuanza kugawa sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili leo katika shule ya msingi Kitangili mjini Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mratibu wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO),Venny Raymond akielezea namna walivyowapata watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kitangili na Kizumbi
Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim akizungumza wakati wa zoezi la kugawa sare hizo za shule

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...