THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KAMISHNA WA TUME YA UCHAGUZI NCHINI KENYA ROSELYN AKOMBE AJIUZULU

Na Mashirika ya Kimataifa.
KAMISHNA wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu, siku saba kabla ya Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba  26, 2017

Akombe ametoa tangazo hilo akiwa jijini New York nchini Marekani, na kusema kuwa hawezi kuendelea kufanya kazi katika Tume hiyo, aliyoielezea kugawanyika.

Aidha, amedokeza kuwa mazingira ya sasa ya kisiasa hayawezi kuruhusu kufanyika kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.

“Siwezi kuendelea kufanya kazi, katika mazingira kaa haya, kila dalili zinaonesha wazi kuwa Uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki,” alisema Akombe akiwa Marekani.

Bi Akombe aliondoka nchini Kenya  siku ya Jumanne, kwenda Dubai kushuhudia uchapishwaji wa karatasi za kupigia kura lakini akaamua kwenda nchini Marekani, ambako pia ni raia wa nchi hiyo.

Kujiuzulu kwa Bi. Akombe, ni pigo kwa Tume hiyo ambayo ilikuwa inamtegemea kuzungumza kwa niaba yake na kuitetea mara kwa mara.

"Tume ijitokeze wazi, iwe na ujasiri na kusema kuwa Uchaguzi huu hauwezi kuwa huru na haki katika mazingira haya," aliongeza Akombe.

Amesema pia alikuwa anapata vitisho kuhusu maisha yake na huenda asirejee nchini Kenya katika siku za hivi karibuni.

Suba Churchil, kiongozi wa mashirika ya kiraia amesema hali hii inaendelea kuzua wasiwasi kuhusu Uchaguzi huo uliopangwa kufanyika wiki ijayo.