Na Bashir Yakub.

napopekuliwa yapo mambo ambayo usipoyazingatia wewe unayepekuliwa basi yatakuingiza matatani mbeleni au hata kama umebambikiziwa kosa itaonekana ni kweli na waweza kwenda jela bila kuwa umetenda kosa lolote.

Kawaida wanaopekua ni askari. Usitarajie huyu anayekuja kukupekua awe ndiye wa kukwambia haki zako . Badala yake wewe unayepekuliwa ndiye uwe wa kumwambia askari kuwa hiki ndicho hiki hapana.

Askari anapokuja kukupekua tayari wewe unashukiwa na hivyo ni rahisi kwake kuacha kufuata au kuongeza jambo lisilokubalika ilimradi atimize lengo lililomleta. Wewe ndiye wa kusema hili ndio na hili hapana. 

Hivyo basi ni muhimu sana kwako kujua kuhusu kupekua na mambo gani ya msingi ufanyiwe au usifanyiwe ili kuepuka uwezekano wa kwenda jela bila kosa. 

Usiseme mimi sina haja ya kujua kuhusu kupekua kwasababu ni mwema sana na hivyo si rahisi kutakiwa kupekuliwa. Laa hasha, kupekuliwa na kukamatwa na polisi humkumba yeyote awe mwema ama vinginevyo. Kujua ni silaha na hivyo ni muhimu kukaa na silaha hii. 

Makala yatapitia sura ya 20, vifungu vya 38 hadi 45 vya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai . 

1. NANI ANARUHUSIWA KUKUPEKUA.

Askari ndiye anayeruhusiwa kukupekua. Hata raia wanaweza kumzuia raia mwenzao wakampekua ikiwa wana taarifa kuhusu kuficha au kumiliki kitu ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria. Isipokuwa ni haramu kabisa kwa raia kumpekua raia mwenzake bila kuwa na kibali maalum. 

2. VITU GANI VINAWEZA KUPEKULIWA. 

Mtu kama mtu anaweza kupekuliwa, kwa maana nguoni mwake kama mifukoni nk. Pia vifaa kama gari, ,meli, nk navyo vyaweza kupekuliwa. Halikadhalika nyumba kama nyumba nayo yaweza kupekuliwa pamoja navyo vifaa vingine. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...