Na Dotto Mwaibale, Muleba, Kagera 
Imeelezwa kuwa Usambazaji wa mbegu za mazao ya mizizi na Migomba kwa vikundi vya wakulima kwenye Mkoa wa Kagera utasaidia kuwahakikishia wananchi wa mkoa huo usalama wa chakula na mazao mbadala baada ya zao lao kuu la chakula la mgomba kuathiriwa na ugonjwa wa mnyauko. 
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Kilimo Mkoa wa Kagera, Louis Baraka wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji wa mbegu bora za mazao hayo kwenye wilaya tano za mkoa huo ambazo ni Missenyi, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Muleba. 
 Alisema kuwa wakazi wa mkoa huo wamekuwa na njaa kali kwa misimu miwili iliyopita kutokana na zao lao kuu la chakula la migomba kushambuliwa na ugonjwa hatari wa mnyauko na hivyo kuwafanya wananchi kuhangaika kutafuta chakula na kuomba chakula cha msaada kutoka Serikalini. 
 Baraka alisema kuwa upatikanaji wa mbegu bora za migomba safi iliyozalishwa kwa njia ya chupa itafufua zao hilo ambalo wakulima wengi walishalitelekeza kabisa baada ya kuona zao hilo likikauka na kushindwa kuwapatia chakula walichokizoea kwa miaka mingi. 
 Aidha Baraka ameishukuru Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo OFAB kwa kuwapelekea pia mbegu bora za Mihogo aina ya Mkombozi na Mbegu bora za viazi lishe ili kuwapatia wananchi wa mkoa huo mazao mbadala baada ya kutegemea zao la mgomba pekee. 
 Alisema kuwa kwenye wilaya zote tano za mkoa wa Kagera COSTECH imeweza kuwapatia mbegu za marando ya viazi lishe 30,000, Mihogo mbegu 27,000 na Migomba 1,000, ingawa wameongea na wafadhili hao na kuwaahidi kuwaongeza mingine zaidi ya 500. 
Kaimu Ofisa Kilimo Wilaya ya Muleba,  Kokushubila Pesha akipanda mbegu ya muhogo katika shamba darasa la kikundi cha Ujamaa  lililopo Kata ya Magata Karutanga wilayani humo. 

Ofisa Mtendaji wa kata ya Magata Karutanga Joyce Rassia akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa shamba darasa la kikundi hicho.

Mjumbe wa kikundi cha Ujamaa,  Liberatha Lespicius akisoma risala wakati wa uzinduzi huo mbele ya mgeni rasmi.

Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku,  Jojianas Kibula akitoa maelekezo kwa wakulima jinsi ya kupanda mbegu hizo bora za mihogo kwa wakulima wa kata ya Magata Karutanga wilayani Muleba.

Baadhi ya wana kikundi cha Ujamaa wakishirikiana kwenye kupanda mbegu hizo bora baada ya uzinduzi rasmi wa shamba darasa hilo. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...