Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mgombea Udiwani wa kata ya Saranga Wilaya ya Ubungo katika uchaguzi mdogo kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) ,Haroun Mdoe amechukua fomu rasmi katika ofisi ya Mtendaji wa kata hiyo leo.
Mdoe amechukua fomu hiyo leo mchana akiwa amesindikizwa na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya kata ya Saranga ambapoiZoezi hilo la uchukuaji fom lilifanyika katika ofisi ya afisa mtendaji kata ya saranga Ndandasi Kijo ambae ni kaimu Mkurungenzi wa uchaguzi katika kata hiyo.
Katika marudio hayo ya uchaguzi vyama mbali mbali navyo vimejitokeza kuchuku fomu hizo ikiwemo chama cha demokrasia na maendeleo( chadema), chama cha wanachi cuf, Act wazalendo, n.k
mara baada ya kuchukua fomu hiyo afisa Mtendaji huyo Kijo alipiga marufuku kufanyika kwa kampeni za aina yoyote kwani mda wa kampeni bado na hivyo yoyote akibainika anafanya kampeni shelia kali zitachukuliwa dhidi ya chama hicho pamoja na mgombea wake.
Katibu wa wilaya ya Ubungo, Salum Kali akimkabidhi barua ya uteuzi kwa mgombea Udiwani wa kata ya Saranga kupitia CCM Mdoe Katika uchaguzi mdogo unaotaraji kufanyika wilaya ya Ubungo
Mgombea Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Saranga, Horoun Mdoe akimkabidhi mtendaji wa kata barua ya uteuzi wake kupitia CCM.
Mgombea Udiwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Saranga Wilaya ya Ubungo, Haroun Mdoe akisoma kwa umakini barua yake ya uteuzi kupitia chama chake cha ccm
Baadhi ya viongozi walio ambatana na mgombea wakati wa kuchukuo fomu wakiwa katika picha ya pamoja
--
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...