UONGZI wa Shamba la Kahawa la Aviv, lililoko kijiji cha Lipokela, kilomita 45 kutoka Songea mjini, umesema Mradi wa umeme wa Makambako-Songea utaleta nafuu kubwa ya kupunguza gharama za kuendesha majenereta ya kufua umeme kwenye shamba hilo kwa asilimia 70, Meneja wa shamba Bw.Hamza Kassim amesema.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea shamba hilo ili kupata maoni ya wamiliki kuhusiana na mradi mkubwa wa umeme wa 220kV, Makambako- Songea Oktoba 12, 2017, Bw. Kassim alisemamahitaji ya umeme kwenye shamba hilo ni Megawati 2.25 hadi 2.5 na zote hizo zinazalishwa na umeme wa kutumia mafuta (Jenereta). 

shamba hilo linalo ilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited yenye makao yake makuu nchini Songapo, lina ukubwa wa Hekta 1,012 kati ya hizo, Hekta 1,000,000 zimepandwa mazao.“Mimea ya Kahawa ambayo imefikia hatua ya kupevuka (matured), ni Hekta 800, huku Hekta 200 bado ni Kahawa changa, tunatumia nishati ya umeme kwa shughuli za umwagiliaji na ubanguaji wa Kahawa ambapo kwa siku tunatumia lita 4,000 za dizeli kuendesha jenereta hizo.” Alifafanua Bw. Kassim.

Ujio wa mradi huu ni faraja kubwa kwetu na tunashukuru mradi huu utakapokamilika utatupunguzia gharama za uendeshaji kwa asilimia 70 na hivyo kutupa fursa ya kufanya upanuzi zaidi wa kilimo cha kahawa, Alibainisha Meneja huyo.
Meneja wa Shamba la Kahawa, Aviv, linalomilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited lililoko kijiji cha Lipokela, kilomita 45 kutoka Songea mjini Bw.Hamza Kassim, (katikati), akizungumzia mradi wa umeme wa Makambako-Songea ambao utaunganishwa kwenye kiwanda chake, mbele ya wahariri wa vyombo vya habari waliofika kiwandani hapo ili kujionea manufaa yatokanayo na mradi huo katika uwekezaji mkubwa, Oktoba 12, 2017.
Meneja wa Mradi wa umeme wa 220kV, Makambako-Songea Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme cha Songea ambacho kiko katika hatua ya ujenzi wa msingi wa kufungia mitambo. Chini ya mradi huo jumla ya vituo vipya viwili vya kupoza umeme vinajengwa huko Madaba na kimoja kinafanyiwa upanuzi huko Makambako
Taswira ya ujenzi wa msingi wa kufungia mitambo kituo kipya cha kupoza umeme cha Songea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...