Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi huyo alisema katika maadhimisho hayo NBC imezidi kuboresha ubora wa huduma na bidhaa mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wateja wao wa kada zote. Kulia ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi wakikata utepe ili kurusha ‘puto’ kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC jijini Dar es Salaam jana.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akizungumza waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo  katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...