Waogeleaji kutoka nchi mbalimbali pamoja na Tanzania waki-dive katika mashindano ya Cana Kanda ya tatu yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.

Kocha wa timu ya Tanzania, Michael Livingstone akisimamia mazoezi ya timu ya Tanzania katika mashindano ya Cana Kanda ya tatu yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.

Na Mwandishi wetu
SERIKALI imeahidi kujenga mabwawa 10 ya kisasa ya kuogelea kwa ajili ya kuendeleza mchezo huo hapa nchini.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hapa nchini, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kanda ya tatu ya Afrika yanayoandelea kwenye bwawa la shule ya Kimataifa ya Heaven of Peace (Hopac).

Waziri Mwakyembe alisema kuwa wamefarijika sana na vipaji vya waogeleaji wa Tanzania katika mashindano hayo ambayo yameshirikisha jumla ya nchi sita ikiwemo ya Tanzania. Nchi nyingine ni Kenya, Uganda, Sudani, Afrika Kusini na Zambia.

“Nimesikitika sana kusikia kuwa kuna wawekezaji walikuja hapa kutaka kujenga bwawa la kuogelea kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huu na kukatishwa tamaa na baadhi ya watendaji wa wizara yangu,”

“Nawaahidi kulishughulikia suala hili kabla ya mwisho wa mwezi huu, nitakutana na Waziri wa Tamisemi na kuona ugumu upo wapi hasa kwa shule maarufu ya msingi ya Oysterbay ambayo ilikuwa iwe ya kwanza kujengewa bwawa la kisasa la kuogelea,” alisema Waziri Mwakyembe.

Alisema kuwa malengo yake ni kuona mchezo wa kuogelea unafikia kiwango cha juu kabisa kwani amegundua nchi ina vipaji vingi, lakini wanashindwa kufikia kiwango cha juu kutokana na kukosa miundombinu ya kisasa.

Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka aliipongeza serikali kwa ahadi hiyo ambacho ni kilio chao cha siku nyingi.

“Tumefarijika sana na ahadi za serikali, kama mnavyojua, tumekuwa tukiangaikia suala la kupata bwawa la kisasa la kuogelea miaka mingi, naamini mafanikio ya ahadi hiyo yataleta msisimko mpya kwa waogeleaji na wadau wake,” alisema Namkoveka.

Namkoveka pia aliwapongeza wachezaji wa Tanzania kwa kuanza kwa vishindi mashindano hayo na kutwaa medali 21 ambapo, nane ni za dhahabu. Waogeleaji, Sonia Tumiotto na Natalie Sanford kila mmoja alitwaa medali mbili za dhahabu katika mashindano hayo.

Waogeleaji wengine waliotwaa medali za dhahabu I Elia Imhoff, Emma Imhoff, Behnson Tara, Marin De Villard na timu ya relay kupitia kwa Collins Saliboko, Hilal Hilal, Sonia Tumiotto na Emma Imhoff.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...