Ofisi ya Msajili wa NGOs inapenda kuujulisha umma kuwa imesimamisha shughuli za Shirika la COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY (CHESA) kuanzia tarehe 20 Oktoba, 2017 ili kupisha uchunguzi unaofanywa dhidi ya tuhuma za shirika tajwa kujihusisha na uhamasishaji wa vitendo vya ndoa za jinsia moja katika maeneo mbalimbali nchini. 

Shirika tajwa pamoja na tuhuma mbalimbali zilizopo, linatuhumiwa kuratibu warsha kuhusu masuala ya ndoa za jinsia moja tarehe 17 Oktoba, 2017 katika hoteli ya Peacock, Ilala – Dar es Salaam.

 Kwa taarifa hii uongozi wa Shirika unaagizwa kusimamisha shughuli zake zote ikiwa ni pamoja na kufunga ofisi zote za Shirika hadi uchunguzi utakapokamilika. Ikumbukwe kuwa ndoa za jinsia moja hazikubaliki nchini kwani ni kinyume na mila, desturi na sheria za nchi.

M.S. Katemba
MSAJILI WA NGOs

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...