Na Thobias Robert

Naibu Waziri wa Ujenzi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kwandikwa ameitaka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kukusanya na kutumia madeni zaidi ya bilioni 10, inayozidai taasisi, idara na wakala mbalimbali wa sekta za umma na binafsi ili watumie pesa hizo katika shughuli za uzalishaji na maendeleo.

Waziri ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi kuongea na kuangalia utendaji kazi wa wafanyakazi pamoja na kukagua mitambo inayotumiwa na wakala hiyo iliyo chini ya wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

“Madeni ni rasilimali ambayo tunahitaji kuisimamia vyema, chambueni vizuri madeni ambayo taasisi inadai kwenye taasisi, idara na wakala mbalimbali za serikali ili tuweze kuona namna gani tutafanya ili madeni hayo yalipwe, kwa sababu tukikaa na madeni mengi yatatukwamisha katika shughuli zetu,” alisisitiza Waziri Kwandikwa.

Aidha alisema kuwa wakala na idara zinazofanya kazi na TEMESA zinapaswa kulipa madeni wanayodaiwa ili kuiwezesha taasisi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kutumia vifaa na miundombinu ya kisasa inayoandana na utoaji wa huduma unaofanya na TEMESA.

“Nitoe wito kwa taasisi mbalimbali zinazodaiwa na TEMESA ziweze kulipa haraka hayo madeni ili tuweze kufanya kazi vizuri zaidi, maana wangekuwa wanakwenda kwenye kampuni binafsi kama wanadaiwa basi magari yao yangekuwa yanakamatwa, sasa isije tukafika wakati na sisi kuanza kampeni ya kuzuia magari, kwa sababu lazima TEMESA isimame ili tuweze kutoa huduma vizuri,” aliongeza Waziri Kwandikwa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa (kulia) akipata maelekezo toka kwa Meneja Msaidizi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Peter Bongele (katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Joseph Nyamuhanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Joseph Nyamuhanga (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa (katikati) kuzungumza na watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mussa Ngwatu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa (katikati) akizungumza na watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Joseph Nyamuhanga na kulia ni Mtendaji.Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mussa Ngwatu.
Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...