Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Richard Mayongela leo akiongea na baadhi ya viongozi wa Matawi ya
Chama cha Wafanyakazi mahala pa kazi (TUGHE), TAA Makao Makuu na Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi mahala pa Kazi (TUGHE) matawi
ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Makao Makuu (TAA HQ) na Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jana wakimsikiliza kwa makini Kaimu
Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard Mayongela (kushoto) alipokutana nao leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania
(TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati mstari wa mbele), akinyanyua mikono juu
kuashiria mshikamano daima na baadhi ya viongozi wa matawi wa chama cha
wafanyakazi mahala pa kazi (TUGHE) matawi ya Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), alipokutana nao leo.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard
Mayongela amewataka viongozi wa wafanyakazi kupitia matawi mawili ya Chama cha
Wafanyakazi, TAA Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), kutenda haki kwa kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi wote bila kubagua na
kuwasilisha kwa mwajiri ili yaweze kufanyiwa kazi kwa wakati.
Bw. Mayongela ametoa kauli hiyo leo wakati viongozi wa matawi hayo walipokwenda
kujitambulisha ofisi kwake TAA Makao Makuu, ambapo alisisitiza kuwa wafanyakazi wa chini
ndio wenye matatizo makubwa lakini wamekuwa hawasikilizwi na kutatuliwa matatizo yao kwa
wakati.
“Ninashukuru uongozi mmekuja kuonana nami, ninahitaji ushirikiano wenu kama chama cha
wafanyakazi, muwatumikie wafanyakazi kwa kutenda haki mkisikiliza matatizo ya kila mmoja
na kufikisha sehemu husika na ninawaahidi kuwa nanyi bega kwa bega kutatua matatizo ya
wafanyakazi kwani wao ndio wanafanya TAA iwepo, endapo wakifanya kazi bila manung’uniko
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...