Mkurugenzi wa Marie Stopes Eng Anil Tambay akielezea namna walivyoweza kutoa huduma ya upimaji wa saratani ya mlango wa shimgo ya kizazi kwa wanawake nchini wakiwa wameweza kupima jumla ya wanawake 187,267 na asilimia 4.2 sawa na wanawake 7,783 wakikutwa tayari wana mabadiliko ya awali ya dalili za saratani ya mlango wa kizazi kwa kipindi cha miaka mitano waliyofanya kazi sambamba na Shirika la PSI Tanzania na Chama cha Uzazi na Malezi (UMATI)

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SERIKALI imenunu vifaa tiba 100, vya tiba mgando ya mabadiliko ya awali ya 
saratani ya mlango wa shingo ya kizazi (cryotheraapy) huku Tanzania ikiwa kinara wa 
ugonjwa huo Afrika.

Hayo yalibainishwa leo wakati wa kufungwa kwa mradi wa uchunguzi na 
matibabu ya awali ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi uliofanyika miaka 
mitano kwa ushirikiano wa Chama cha Wazazi na walezi(UMATI), PSI na Marie Stopes kwa uwezeshwaji wa taasisi ya Bill and Gates.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mama na Mtoto 
kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk Safina 

Yuna, amesema mradi huo umesaidia kuboresha upatikanaji wa mabadiliko ya 
saratani ya mlango wa shingo ya kizazi katika vituo 90.

"Kama mnavyojua Tanzania inaongoza kwa saratani ya mlango wa kizazi hawa 
wametusaidia, Serikali imeamua kupanua wigo na kupunguza gharama za 

matibabu kwa wagonjwa."amesema.

Amesema takwimu zinaonesha kuwa wagonjwa wengi hufika hospitali ya Ocean 
road wakiwa katika hatua za mwisho ambapo matokeo ya matibabu yanakuwa 

si mazuri huku akibainisha mgonjwa akiwahi hupona.

Amesema vifaa tiba hivyo vitatumika kutibu matibabu ya awali na upasuaji 
mdogo kwa wagonjwa wenye mabadiliko makubwa ambapo tayari 
vimeshasambazwa katika vituo 466 hapa nchini .

"Tutatanua zaidi kuhakikisha huduma hizi zinawafikia walengwa wengi ambao 
hawawezi kufika katika hospitali za wilaya na Mikoa pamoja na vituo vya afya 

nchini."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mifumo ya Afya ya Marie Stopes, Jeremia 
Makula amesema mradi huo umefika katika mikoa 22 nchi nzima katika vituo 
61 vilivyokuwa vikitoa huduma.
"Katika kipindi cha maiaka 5 tuliwafikia wanawake 187,267 katika uchunguzi 
wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi na tumegundua asilimia 4.2

walikuwa na mabadiliko ya awali ya kansa ya kizazi,"amesema.

Ameongeza kuwa wametibu wanawake 7600 sawa na asilimia 100 ya 
waliokuwa wakihitaji matibabu ya awali ya mabadiliko ya awali ya saratani ya 
mlango wa shingo ya kizazi. 
Amesema wanawake 1000 wamekuwa wakihitaji huduma ya juu huduma 
ambapo walipewa rufaa ya matibabu katika hospitali zinazotoa huduma hiyo.

Makula amesema katika mradi huo wameanza kutumia kipimo kipya ambacho 
hakijawahi kutumika hapa nchini licha ya kuwa na changamoto nyingi katika 
kuwafikia waliokuwa vijijini.

Mkurugenzi wa masuala ya uzazi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Safina Yuna akizungumza namna seriakali walivyoweza kuongeza vituo na kufikia 436 nchi nzima na kuongeza vifaa tiba 100 kwa ajili ya matibabu ya awali  katika hospitali za Wilaya na Mkoa na juhudi hizo ni katika kupunguza ongezeko la saratani ya mlango  wa shingo ya kizazi kwa wanawake nchini.
t
Dr Mary Rose Kahwa Giattas kutoka shirika la JHPIEGO linalojishughulisha na masuala ya udhibiti wa saratani ya kizazi wakishirikiana na serikali akitoa pongezi kwa Shirika la PSI Tanzania , Chama cha Uzazi na Malezi (UMATI) na Marie Stopes kwa juhudi kubwa walizozifanya kwa kutoa huduma ya upimaji wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi kwa wanawake kwa kipindi cha miaka mitano, Kulia ni Mshauri wa masuala ya udhibiti wa wa kansa ya kizazi Dr. Robert Kamala na kushoto ni mratibu wa masuala ya udhibiti wa wa kansa ya kizazi Dr. Edwin Swai.
Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi kutoka Shirika la PSI Tanzania Prudence Masako akizungumza nama walivyoshirikiana na Chama cha Uzazi na Malezi (UMATI) pamoja na Marie Stopes katika kuwasaidia wanawake wenye matatizo ya saratan ya mlango wa shingo ya kizazi sambamba na changamoto walizokutana nazo kwenye miaka mitano ya mradi wao ambapo wanawake wengi wameshindwa kupata huduma zinazostahiki kutokana na kukosa fedha za matibabu,pia kwenye vituo vyao takribani 22 wamekuwa wanahudumia wanawake wasiozidi 20 kwa mwezi mmoja.
Dr Lugano Daimon kutoka  Chama cha Uzazi na Malezi (UMATI) akielezea namna walivyoweza kushirikiana na Shirika la PSI Tanzania na Marie Stopes katika kutoa huduma ya upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwa miaka mitano na kupitia vituo vyao 11vilivyopo nchini wamepima jumla ya 81,802 na katika hao jumla ya wanawake 2,862 sawa na asilimia 3.5 wakutwa tayari wana viashiria vya saratano ya mlango wa shingo ya  kizazi.
Baadhi wa washiriki kutoka sehemu mbalimbali wakiwa wanafuatilia mkutan huo wa ufungwaji wa mradi wa miaka mitano wa kutoa huduma ya kupima saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake nchini uliokuwa chini ya Shirika la PSI Tanzania, Chama cha Uzazi na Malezi (UMATI) na Marie Stopes.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...