WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani aliyasema hayo leo katika kikao cha pamoja baina yake na uongozi wa shirika hilo wakiwemo wadau ambapo alisema watahakikisha wanawahudumia wateja kwa wakati ikiwemo uhakika wa vifaa vyenye bora ili kuwawezesha wananchi kupatiwa umeme kwa haraka zaidi.
Licha ya hivyo lakini pia Waziri huyo alitilia mkazo suala la madeni yote ya bili za umeme kulipwa kwa wakati kwenye shirika hilo ili kuweza kuwezesha ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi.
Akizungumza na wazabuni mbalimbali wa miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo,nyaya na mita,Waziri Kaleman alisema kuanzia sasa vifaa vya umeme vitanunuliwa ndani ya nchi kwani kufanya hivyo itapunguza gharama kubwa na kasi ya kuwahudumia wateja."Kwani kufanya hivyo vifaa hivyo vitakuwa karibu kupatikana ndani ya nchi na kutaongeza mapato ndani ya nchi na uzalendo "Alisema.

Hata hivyo alilipongeza shirika la Umeme nchini Tanesco kwa kufanya kazi kwa bidii na kutoa taarifa kwa wateja juu ya huduma mbalimbali ikiwemo kuwataka kuwajibika kwa kufanya kazi kwa waledi mkubwa.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na uongozi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco na wadau wa mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa uhakika ikiwemo kuwahudumia wateja kwa wakati na kuwepo kwa uhakika wa vifaa vyenye ubora ili kuwezesha 
Naibu Waziri wa Nishati  Mhe. Subira Mgalu akizungumza katika kikao hicho 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo akiongea katika kikao hicho kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani 
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kaleman akiambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Subira Mgalu wamefanya kikao na uongozi wa shirika la Umeme nchini (Tanesco) na wadau mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha nishati ya umeme wa uhakika unapatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...