Na Ramadhani Ali – Maelezo

Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini kutoka nje wameshauriwa kutoogopa gharama wakati wa kusafirisha bidhaa zao na wahakikishe wanatumia njia bora za usafirisha ili mizigo yao ifike ikiwa salama.

Mkuu wa Idara ya Udhibiti na usalama wa chakula wa Bodi ya Chakula na Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Khamis Ali Omar ametoa ushauri huo wakati wa kuangamiza tani 11.6 za maziwa katika dampo la Kibele yaliyoingizwa nchini baadhi yakiwa yameharibika kutokana na usafirishaji mbaya.

Alieleza kuwa sehemu ya maboksi ya maziwa yalipasuka na kuharibu mengine na baada ya kuyafanyia uchunguzi walijiridhisha kuwa yalikuwa hayafai kwa matumizi ya binaadamu.Alisema waliishauri Kampuni iliyoiingiza maziwa hayo Farid Supply kuyarejesha yanakotoka ama kuyaangamiza baada ya kuona yako katika hali hatarishi ya afya za wananchi na walikubali yaangamizwe ili kupunguza gharama ya kuyarejesha.

Dkt. Khamis aliwataka wafanyabiashara kuelewa kuwa kunatafauti kubwa ya kusafirisha vyakula vya maji maji na bidhaa nyengine za kawaidi na vyakula vya maji maji vinahitaji tahadhari kubwa zaidi wakati wa kusafirishwa.Alisema lilijitokeza katika kusafirisha maziwa hayo ni kukosekana umakini na kusababisha kontena lililobeba maziwa kuserereka wakati wa safari na baadhi ya maboksi yalianguka na kuapasuka nadani ya kontena hilo.

Meneja wa Kampuni ya Farid Supply Mansour Said ambae alishiriki katika zoezi hilo Kibele, alikubali kuwa kulitokea tatizo katika kontena hilo na baadhi ya maboksi ya maziwa yalipasuka lakini sehemu kubwa ya maziwa hayo yalikuwa hayajaharibika na yalikuwa yanafaa kutumika.

Alisema maziwa hayo yaliyokuwa na thamani ya zaidi ya sh. 52 milioni huenda yalianza kuharibika baada ya kuzuiliwa kwa kwa kipindi cha miezi nane katika bandari ya Zanzibar .
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakishusha maziwa tani 11.6 na bidhaa mchanganyiko zilizo haribika kwa ajili ya kuangamizwa katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
Gari la Kijiko likiangamizwa maziwa yaliyoharibika pamoja na bidhaa mchanganyiko katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Idara ya Udhibiti na Usalama wa chakula Dkt. Khamis Ali Omar (wambele) akisimamia ungamizwaji wa bidha zilizoharibika katika dampo la Kibele.
Meneja wa Kampuni ya Farid Supply iliyoingiza maziwa hayo Mansour Said akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu ya sehemu ya maziwa hayo kuharibika.Picha na Makame Mshenga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...