KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto amewataka watoa huduma na mafunzo kuhusu lishe bora yaanzie ngazi za shule ya msingi ili kuwajenga watoto kuzingatia mlo bora katika kukuza afya za watanzania. Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).

“Walimu wawe sehemu ya afua za kufundishia wanafunzi juu ya lishe bora hasa kuanzia ngazi za shule ya msingi ili kuwajengea mazoea watoto kupenda kula mlo ulio bora hata wanapokuwa majumbani mwao” alisema Dkt. Ulisubisya. Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa baadhi ya watoto walio vijini na mijini wana utapia mlo kwa kukosa chakula kilicho bora hivyo jamii inatakiwa izingatie lishe bora ili kuimarisha afya za watoto nchini.

Mbali na hayo Dkt. Mpoki amesema kuwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawe kipaumbele katika kutoa elimu ya lishe bora ili kuweza kujikinga na Unyafuzi, Kwashakoo na magonjwa yasiombukiza kama vile Kisukari,shinikizo la damu ,magonjwa ya moyo yanayotokana na ulaji kupita kiasi.

Kwa upande wake Meneja wa Magonjwa yasioambukiza ,Usalama wa Chakula na lishe ECSA Bi. Rosemary Mwaisaka amesema kuwa wameamua kuandaa vitini na vitita vya kufundishia lishe bora ili kuweza kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kufikisha elimu hiyo kwa walengwa.

“Tumeamua kuandaa vitini hivi ili viweze kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kuweza kuwafundisha wanajamii juu ya umuhimu wa kula mlo bora na vitatumika Kenya,Uganda na Tanzania” alisema Bi. Mwaisaka. Mbali na hayo Mshiriki wa Mafunzo ya Lishe bora kutoka ECSA ambae pia ni Mtoa huduma Bi. Evelyne Minja amesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kutoa huduma katika jamii kuhusu mlo bora hasa kwa watoto vijijini na mijini.

“Mafunzo haya yametufanya tujue jinsi ya kuwahudumia na kutoa ushauri juu ya mlo bora hasa kwa watoto wenye viashiria vya utapia mlo kwa kuwapima na kuwapangia vyakula vinavyostahili” alisema Bi. Minja.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wadau mbalimbali wa maswala ya lishe hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kushoto akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Vincent Assey wa kwanza kulia wakati wa uzinduzi wa hivyo vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kulia akikata keki kuashiria kuzindua vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Afisa msaidizi wa ECSA Bi. Dorin Marandu.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kulia akimlisha keki mmoja wa washiriki na mtoa huduma wa lishe ngazi ya jamii Bi. Evelyne Minja wa pili kushoto wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam. PICHA NA ALLY DAUD -WAMJW.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...