THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Dkt.Ndugulile afungua kambi ya upasuaji Mabusha mkoani Lindi

 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 264 toka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Statoil bw.Oyotein Michelsen .Fedha hizo ni kwa ajili ya kambi za upasuaji wa mabusha na ngirikokoto kwa watu wapatao 400 kwa mwaka 2017 na 2018. Kulia ni Mkurugenzi wa Kinga toka Wizara ya Afya Dkt.Neema Rusibamayila ambapo Mpango wa Taifa wa kutokomeza Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele ndiye mratibu wa upasuaji huo
 Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile akihutubia wananchi waliofika kwenye uzinduzi wa upasuaji wa mabusha na ngirikokoto kwa wagonjwa wapatao 200 wa Manispaa ya Lindi
 Dkt.Faustine Ndugulile akipokea mashine ambayo ina kisu cha moto ambacho kinazuia damu wakati wa upasuaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Statoil Bw.Oyotein Michelsen.  Kulia ni Mkurugenzi wa Kinga toka Wizara ya Afya Dkt.Neema Rusibamayila ambapo Mpango wa Taifa wa kutokomeza Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele ndiye mratibu wa upasuaji huo
 Mkurugenzi wa Statoil Bw.Oyotein Michelsen akisoma hotuba kwenye ufunguzi wa kambi ya upasuaji inayofanyila kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa Sokoine mkoani Lindi
Baadhi ya wananchi wanaotarajia kufanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo