THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KAMPUNI YA BIMAA YA UAP YATOA FIDIA KWA WAATHIRIWA NA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO MKOANI MBEYAMkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala (kushoto) akimkabidhi mteja wa bima ya Kampuni ya UAP Ndugu Godi Sanga kama fidia kutokana kukumbwa na janga la moto la kuungua kwa Soko la Sido Agosti 15 ,2017
Mteja wa Kampuni ya UAP akikabidhiwa mfano wa hundi ya malipo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala ,ambapo kampuni hiyo ya bima imekamirisha kulipa fidia hizo kwa wateja wake ambapo zaidi ya shilingi milioni 250 zimelipwa huku kiwango cha chini kulipwa katika fidia hiyo ni shilingi milioni Saba huku mteja wa juu kulipwa ni shilingi milioni 180.
Mkurugenzi Mtendaji wa UAP Mick Itunga akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi wateja wa kampuni ya bima ya UAP jana Nov 14 katika viwanja vya soko la Sido jijini mbeya ambapo amesema kuwa UAP ni kampuni kongwe katika sekta ya Bima duniani kwa miaka zaidi ya 170 ambapo amesema kampuni hiyo ndiyo yenye mtaji mkubwa wa Bima Tanzania ikiwa na zaidi ya shilingi Bilioni 20. Aidha Mkurugenzi huyo pia ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara wa mbeya kuendelea kuiamini UAP kama bima bora nchini nakwamba itakuwa mstari wa mbele mara wanapokutwa na majanga ya moto kama yaliyotokea katika soko hilo la Sido jijini Mbeya.
Mfanyabiashara wa Soko la Sido jijini Mbeya Ndugu Godi Sanga ambaye ni mteja wa Bima ya Kampuni ya UAP akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya malipo kutoka kwa kampuni hiyo ya Bima ambapo ametumia fursa hiyo kuishukuru kampuni hiyo kwa kumlipa fidia yake sanjali na kuwataka wafanyabiashara wenzake kuhakkisha wanajinunga na makampuni ya bima ili kujiwekea usalama wa biasahra zao.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika Picha ya pamoja na wadau wa bima.