MASHINDANO ya michezo ya maadhimisho ya siku kuu ya kumbukumbu ya kumuenzi Mtakatifu Gaspari Del Buffalo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya michezo vya kanisa, hatimaye yamefikia tamati,ambapo timu ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari na chuo cha uuguzi iliyopo katika Mji mdogo wa Itigi,wilayani Manyoni imatawazwa kuwa mabingwa wa mpira wa miguu wa mashindano hayo mwaka huu.

Katika mashindano hayo yalizishirikisha jumla ya timu nane za wanaume za mpira wa miguu na mpira wa pete huku kukiwa na malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu zilizoshiriki katika mashindano hayo.

Mmoja wa viongozi wa timu ya mpira wa pete kwa wanawake,Hayfat Hassani aliwashauri waandaaji wa mashindano hayo kwamba kwa kuwa timu nyingi zilizoshiriki hazikuwa na jezi,hivyo aliwataka kuangalia uwezekano wa kuzipatia jezi timu zitakazoshiriki katka mashindano ya mwaka ujao.

Aidha akizungumzia kuondokana na malalamiko ya upendeleo unaofanywa na waamuzi,Hayfat alishauri pia kwamba katika mashindano kama hayo kwa mwaka ujao ni vyema waamuzzi wa michezo hiyo wakatafutwa kutoka nje ya maeneo ya Halmashauri ya Itigi.

“Kwa sababu kulikuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wachezaji kuhusu kocha wa timu yetu ambaye naye alikuwa akichezesha kwenye mashindano hayo kuwa alikuwa hazitendei haki timu zingine pinzani na timu yake wakati zilipokuwa zikichuana huku yeye akiwa mwamuzzi wa mchezo huo”alifafanua Hayfat. 
Ni baadhi ya washiriki wa mchezo wa kuvuta kamba kwenye mashindano ya maadhimisho ya kumuenzi Mtakatifu Gaspari,Itigi,wilayani Manyoni.(Picha Na Jumbe Ismailly).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...