Na Mathias Canal, Arusha

Serikali imekuwa ikiongeza idadi ya wanafunzi katika Vyuo vya Kilimo na kwa sababu hiyo Maafisa Ugani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka ambapo hali hiyo imewezesha Karibu kila Kata hapa nchini kuwa na Afisa Ugani.

Lakini pamoja na kuwepo kwa wataalamu hao wa kilimo bado uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini yakiwemo mazao ya chakula na biashara si wa kuridhisha ambapo wakulima wanalima na kupanda pasina hata kufuata hatua za kitaalamu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi akizungumza na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI TENGERU) kilichopo katika Kijiji cha Tengeru, Kata Patandi, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.

Alisema lengo la Serikali kusambaza Maafisa Ugani kwenye Halmashauri mbali mbali nchini ilikuwa kuwasaidia wakulima waweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi na kuongeza mavuno.

Hata hivyo jambo hilo limekuwa kinyume kwani asilimia kubwa ya maafisa ugani ama hawafanyi kazi zao ipasavyo ama wameshindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akiwasili katika Ofisi za Taasisi ya Horti Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru). Mwingine ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt Mansoor Hussein


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...