Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii kutoka nchini Rwanda, inaeleza kuwa mume wa zamani wa Muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo, Ndikumana ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda, amefikwa na mauti hayo akiwa nyumbani kwake mjini Kigali. 

kwa mujibu wa Uongozi wa timu hiyo umesema kuwa jana Ndikumana ambaye alionekana kuwa bado yuko fiti na haonyeshi dalili zozote za kuumwa alifanya mazoezi na wachezaji wake na baadaye kuagana na kurudi nyumbane kwake, ambapo wamepatwa na mshtuko baada ya kusikia amefariki Dunia. Haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini kwani hakuwa mgonjwa na wala hajapata ajali. 

Mwili wake umepelekwa monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala kwa maombi ya familia yake kwani miili ya waislamu haihifadhiwi katika monchwari za kawaida kwa mujibu wa imani zao. Uwoya na Ndikumana walifunga ndoa mwaka 2009 na kujaaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Krish kisha wakaja kutengana mwaka 2013. 

 Mungu ampe malazi mema peponi - Amin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...