Na Mathias Canal, Dodoma

Serikali imesema kuwa Mpango wa Serikali wa kuwapelekea wakulima wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma mbegu mpya za Kahawa ni mahususi kwa ajili ya kuinua uzalishaji kwa kutekeleza Mpango Mkakati wa Kuendeleza Zao la Kahawa katika kipindi cha miaka 10 yaani mwaka (2011 – 2021).

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) amebainisha hayo leo Novemba 10, 2017 Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mhe Martin Mtonda Msuha (Mb) Aliyetaka kufahamu kuhusu kushuka Kwa takwimu katika miaka ya hivi karibuni ya uzalishaji wa Kahawa Wilayani Mbinga kwa mkulima mmoja mmoja (out growers) ambapo alitaja sababu za mojawapo zilizopelekea kushuka kwa uzalishaji huo kuwa ni pamoja na kuzeeka kwa miti ya kahawa.

Mhe Mwanjelwa alisema kuwa Katika mpango huo, utafiti na usambazaji wa miche bora itatolewa ili kuondokana na miche yenye tija duni na iliyozeeka. Ambapo Utekelezaji wake unafanyika kwa kushirikiana na wadau hususani Tanzania Coffee Research Institute (TaCRI).

Alisema, Kituo cha Utafiti na uzalishaji miche cha Ugano kilichopo Wilayani Mbinga, katika mwaka 2016/2017 kilizalisha na kusambaza miche bora ya kahawa 270,869 na kazi mpaka hivi sasa inaendelea.

Aidha, Mfuko wa Maendeleo ya Kahawa (Tanzania Coffee Developemnt Fund (TCDF) umefadhili na kupunguza bei kutoka shilingi 300 kwa mche mmoja hadi shilingi 150 kwa vituo vyote nchini vilivyoko chini ya TaCRI ili miche hiyo isambae kwa kasi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Leo Novemba 10, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akijadili jambo na Mhe Jenista Joakim Mhagama ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...