Viongozi wa vijiji, kata na tarafa Wilayani Bukombe wametakiwa kutumia michango inayotolewa na wananchi kwa shughuli zilizokusudiwa ili kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao.
Akizungumza katika kijiji cha Kazibizyo kata ya Ng'anzo Wilaya ya Bukombe Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita amesema katika  vijiji, kata na tarafa wananchi wamekuwa wakihimizwa kujitolea kuchanga michango ya hiari ili kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo lakini baada ya michango hiyo kukusanywa inatumika kwa maslahi binafsi ya Viongozi.
Amesema kuwa Viongozi hao wasio na maadili  wanapanga matumzi ya fedha za wananchi bila kujali vipaumbele vya vijiji kwa maslahi yao binafsi vitendo hivyo vinawavunja moyo wananchi wa kutoendelea kutoa michango ya maendeleo. "Kuna vidudu vinavyoleta magonjwa watu wanasubili maendeleo hayatokei inabidi tuvitoe tuvipige sindano kubwa vife humu humu viongozi wa namna hiyo wasio na maadili wamekuwa wakihamishwa wakati hawajatoa taarifa za mapato na matumizi alah! kama yupo Geita arudi arejeshe fedha za wananchi popote alipo".
Amesema kama kuna mtu au mtendaji anayeona hatoshi apishe akae pembeni ili wanaoweza kufanya kazi wafanye ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi. Hata hivyo, ametoa wito kwa wananchi kutumia rasilimali zinazowazunguka kujiletea maendeleo badala ya kukaa na kulalamika maisha magumu wakati kuna rasilimali nyingi katika maeneo wanayoishi.  Aidha, amezitaka Halmashauri Mkoani Geita kusajili na kuvitumia vikundi vya mafundi vinavyojitolea kujenga madarasa na Zahanati bila malipo katika miradi ya fedha katika maeneo mbalimbali ili vijana hao wanufaike badala ya kutoa kazi zote kwa wakandarasi.
Awali  Josephat Maganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa Wilaya ya Bukombe ina vijiji 52 na Vitongoji 372 lakini kuna Zahanati sita (6) tu za Serikali.  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akiwa Wilayani humo amezindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati katika vijiji vya Kazibizyo na Bulama kwa kushiriki katika ujenzi na harambee iliyoleta michango ya mifuko 93 ya simenti, fedha tasilimu  shilingi 340000/=, tofali 500,mbao 50 na misumari kilo3.
 Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita (Aliyevaa kofia usalama) akishiriki kubeba mawe  na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa msingi katika Zahanati ya kijiji cha Kazibizyo Wilayani Bukombe.Wananchi wa kijiji hicho wanatembea umbali wa Kilometa 20 kwenda Ushirombo kupata huduma za afya.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akishirikiana na mafundi wa ujenzi kujenga msingi wa Zahanati ya kijiji cha Kazibizyo alipotembelea kijiji hicho kuzindua kampeni ya ujenzi wa Zahanati na Vyumba vya madarasa.
 Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kazibizyo Wilaya ya Bukombe baada ya uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa Madarasa na Zahanati Wilayi Bukombe.

 Mhandisi Robert Gabriel akishirikiana na wananchi pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Bukombe kuchanganya mchanga na sementi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi kijiji cha Bulama. 
Josephat Maganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bulama wakazi wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kijijini hapo ili kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati. Habari na picha: Magesa Jumapili - Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...