Na John Nditi, Morogoro
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe, amewaonya Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya za mkoa huo ambao watakalia fedha za wananchi wanaojiunga na Mfuko wa Afya  ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa na kuzitumia vinginevyo  wanawajibishwa mara moja.
Dk Kebwe alisema hayo, wakati akifunga kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya Mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro mwanzoni mwa juma hili mjini hapa.
Wajumbe wa kikao hicho walipitia  taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Tuimarishe Afya kunzia  Juni hadi Novemba  2017 pamoja na utekelezaji wa Mradi  ya mkoa  wa Juni  hadi Novemba mwaka huu uliohusu mpango wa uchangaji wa CHF iliyoboreshwa na upatikanaji wa dawa na vifaa  tiba kwenye Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali.
Dk Kebwe aliwataka wakurugenzi hao  wanapopelekewa  makusanyo ya fedha za kaya zinazotokana na wananchi kujiunga  na  CHF iliyoboreshwa,  wajibu ni  kuziingiza kwenye mfumo na kuzipeleka  kwenye vituo  ili zikatumike kununua  dawa na vifaa tiba na si vinginevyo.
Pamoja na  kusema hayo ,aliishukuru Serikali ya Uswiss kupitia Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la nchi hiyo kwa ufadhili wa mradi wa Tuimarishe Afya ambao unachochea uboreshaji wa huduma za afya kupitia mpango wa CHF iliyoboreshwa  unaotekelezwa katika mikoa mitatu ya Shinyanga, Dodoma na Morogoro.
Naye Meneja  mkoa  Mradi  wa Tuimarishe Afya (HPSS) , Dk Harun Machibya alisema kuwa kiwango cha kujiunga na CHF iliyoboreshwa kimkoa imeongezeka kutoka asilimia 3  tangu kuanza kwa mradi huo na kufikia asilimia 11.3 hadi Novemba mwaka huu na mwekezo mzima ni kifikisha asilimia 25 hadi Julai 2018.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa huo, Clifford Tandari alizitaka halmashauri ambazo zinadaiwa fedha na Hospitali ya Rufaa ya mkoa kuwasilisha malipo yao mara moja ili huduma za wananchi ziweze kupatikana kwa ufanisi mkubwa.
Hata hivyo alisema , siku za usoni mpango huo unaunganishwa  kiteknolojia kwa kaya kuweza  kujiunga kuwa  wanachama wa CHF iliyoboreshwa kupitia mifumo ya miamala ya fedha kwa njia ya simu kama ilivyo kwa huduma nyingine za kifedha .
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe,akisisitiza jambo  wakati wa kufunga kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro  wengine waliokaa kwenye meza kuu ni Katibu Tawala wa mkoa , Clifford Tandari  pamoja na Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo.
 Meneja wa Mradi   wa Tuimarishe Afya (HPSS) , Manfred Stoemer ( kulia) akiteta jambo na Kiongozi wa Wataalamu wa Mradi huo, Profesa Manorios Meshack  ( kushoto)  wakati wa kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro.
 Baadhi ya wajumbe wa  kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro  wakisiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi  wakati wa ugufaji wa kikao hicho kilichofanyika mkoani  Morogoro.
 Wakuu wa wilaya za mkoa wa Morogoro  ( mstari wa mbele ) ambao ni wajumbe   kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro  wakisiliza hotuba ya mgeni rasmi  ya  ugufaji wa kikao hicho kilichofanyika , mkoani  Morogoro.
 Mganga  mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk  Frank Jacob akisoma sehemu ya maazimio ya kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro  kabla ya mkuu wa mkoa huo, Dk Kebwe Stephen Kebwe  ( wapili kulia walioketi ) kufunga kikao hicho.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mradi wa Tuimarishe Afya  wa mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja  kabla ya kuanza kwa kikao cha nne cha Bodi ya Ushauri ya mkoa ya Uimalishaji Mifumo ya Sekta ya Afya mkoa wa Morogoro kilichofanyika mkoani  Morogoro.( Picha na John Nditi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...