Na Robert Hokororo, Kishapu DC.
Shirika la Msaada na Mandeleo ya
Jamii (REDESO)
katika Halmashauri ya wilaya ya Kishapu limewapa mafunzo wazalishaji na
wasindikaji wa zao la mkonge kutoka Kishapu na Meatu mkoani Simiyu.
Mafunzo hayo yaliyofanyika ukumbi
wa Halmashauri Kishapu yanalenga kuwajengea washiriki hao uwezo wa utumiaji
rasilimali kwa tija katika kuzalisha na kukidhi mahitaji ya soko la bidhaa
wanazozalisha katika maeneo yao.
Mafunzo hayo yalitolewa kwa pamoja
na Mshauri wa kujitegemea, Steven Tilubuza kutoka Mwanza na Afisa Ushirika
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephano Shadrack.Yanatarajiwa kuwapatia washiriki
hao kutoka vikundi vya ujasiriamali elimu na ujuzi wa namna ya uanzishaji wa
miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali kwenye maeneo hayo.
Meneja wa REDESO Kishapu, Charles
Buregeya alisema washiriki hao kutoka vikundi vya ujasiriamali watanufaika na
mafunzo hayo ambayo yatawajengea uwezo wa kutambua fursa mbalimbali waliko.“Kupitia mafunzo hayo washiriki
wataweza kujikwamua kutoka umaskini na kuwa na fursa nzuri za kujipatia kipato kwani
wataweza kuibua na kuanzisha miradi ya maendeleo,” alisema Buregeya.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa
mafunzo hayo yatasaidia washiriki kupata elimu ya kubaini na kutafuta masoko ya
bidhaa zao wanazozalisha hivyo kupata wigo mkubwa wa wateja.Utaalamu mwingine washiriki
wanaopata kupitia mafunzo hayo ni pamoja na namna ya ufungashaji mzuri wa
bidhaa zilizozalishwa pia kuzitangaza kupitia njia mbalimbali ili ziwafikie
wateja.
Mshauri wa kujitegemea, Steven Tilubuza kutoka Mwanza akitoa mada katika mafunzo hayo yaliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Kishapu.
Meneja wa Shirika la Msaada na Mandeleo ya Jamii (REDESO) Kishapu, Charles Buregeya akitoa ufafanuzi kuhusu mafunzo hayo kwa waashiriki.
Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephano Shadrack akitoa mada kuhusu ushirika katika mafunzo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...