Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imewasilisha Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma.

Muswada huo umewasilishwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Prof. Makame Mbarawa. Wakati akiwasilisha Muswada huo, Mhandisi Nditiye alisema kuwa Muswada huu unapendekeza kutungwa kwa Sheria itakayoanzisha Shirika la Uwakala wa Meli ambalo pamoja na majukumu mengine litakuwa na jukumu la kutoa huduma ya uwakala wa meli na kudhibiti huduma za usafiri na usalama wa vyombo vya majini.

Ameongeza kuwa, Muswada huu utaweka mfumo madhubuti wa uendeshaji wa biashara ya uwakala wa meli na udhibiti wa huduma za usalama wa usafiri wa meli hivyo utaimarisha udhibiti wa sekta ndogo ya usafiri wa meli na kuifanya sekta hii kuchangia vyema katika uchumi na kuongeza pato la Taifa. Muswada huu ni moja ya jitihada za Serikali za kuhakikisha kuwa taasisi zake zinajiendesha kwa faida, kibiashara, kwa ushindani na kutoa gawio kwa Serikali ili iweze kuhudumia wananchi kwa kujenga miundombinu ya kisasa na kuwapatia wananchi huduma mbali mbali za kijamii.

Mhandishi Nditiye aliyataja majukumu ya Shirika kuwa ni pamoja na uhakiki wa shehena inayoingia na kutoka kupitia bandari za Tanzania, uondoshaji shehena za madini, makinikia, wanyama hai, nyara za Serikali, na bidhaa zinazotokana na madini na udhibiti wa watoa huduma katika sekta ndogo ya usafiri majini, usalama wa meli na mazingira ya bahari. 
Naibu Waziri wa Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (mwenye koti) akifuatilia majadiliano baada ya kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli wa Taifa mbele ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Prof. Norman Sigalla King (katikati) akichangia maoni yake kuhusu Muswada huo. Wa kwanza Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Selemani Kakoso.
Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania Mzee Renatus Mkinga (aliyesimama) akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kuhusu Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli wa Taifa kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma. Naibu Waziri wa Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (mwenye koti) akifuatilia majadiliano hayo na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Prof. Norman Sigalla King.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Mhe. Rukia Kassim akichangia maoni yake kuhusu Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli wa Taifa mbele ya Kamati hiyo na wadau wa sekta ndogo ya usafiri wa majini kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...