Shirika la kimataifa la Save The Children limetoa msaada wa pikipiki kwa ajili ya dawati la jinsia na watoto la jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 10,2017 wakati wa kukabidhi pikipiki moja kwa jeshi la polisi,Meneja wa shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga Benety Malima alisema pikipiki hiyo itasaidia katika ufuatiliaji wa makosa mbalimbali yakiwemo ya jinai. 

“Shirika letu limekuwa likiendesha mafunzo kuhusu ukusanyaji wa vielelezo kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi kwa ushahidi mahakamani,tumebaini kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo ni usafiri,kutokana na hali hiyo tumeona tuangalie namna ya kuwezesha usafiri ili kukabiliana na vitendo vya ukatili katika jamii”,alieleza Malima. 

Akipokea pikipiki hiyo SSP Lutusyo Mwakyusa aliyemwakilisha kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule,alilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kusaidia jeshi la polisi. 

“Tunalishukuru shirika la Save the Children, huu ni msaada mkubwa sana kwetu kwani utasaidia kuokoa maisha ya watu,na hiki ni kielelezo tosha cha ushirikiano kwa vitendo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia,naomba wadau wengine waige mfano wa shirika hili ili kujenga jeshi letu la polisi”,alieleza Mwakyusa. 

Aliwataka wadau kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa matukio ya ukatili yanatokomezwa. 
Pikipiki iliyotolewa na shirika la Save The Children kwa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ili itumiwea na dawati la jinsia na watoto kufuatilia matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi pikipiki kwa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya dawati la jinsia na watoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...