WARSHA ya Kimataifa ya wanachama wa Umoja wa Posta Afrika kwa nchi zinazozungumza Kiingereza, imefanyika jijini Arusha, Tanzania ikizishirikisha nchi mbalimbali barani Afrika.

Katika warsha hiyo, ijulikanayo kama ‘operational readness for e-commerce,’ ilianza Novemba 6 na kumalizika Novemba 8, 2017, Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete, aliwataka kuwa na utayari wa kibishara ili waweze kuendana na mabadiliko ya tekinolojia.

"Tukiongeza ubunifu wa kufanyakazi kwa mbinu za kisasa kwa kutumia huduma za intaneti, wateja wengi watavutiwa na kuendelea kuwepo kwenye soko na kuweza kukabiliana na ushindani wa kibishara." Alisema.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete, akizungumza wakati akiifungua warsha ya kimataifa ya wanachama wa Umoja wa Posta Afrika kwa nchi zinazozungumza Kiingereza, ilioanza jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Mount Meru, Novemba 6 na kumalizika Novemba 8, 2017.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta duniani (UPU), Bi. Loilinda Dieme, akizungumza katika warsha hiyo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Bw. Younous Djibrine, akizungumza katika warsha hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Deo Kwiyukwa akizungumza katika warsha hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...