NA DENIS MLOWE, IRINGA

WAZAZI na Walezi wameaswa kuwasomesha watoto wa kike na kuachana na fikra potofu kuwa kumsomesha mtoto wa kike ni kupoteza rasilimali fedha kwani maisha ya sasa bila elimu ni changamoto kubwa kwa mtoto wa kike.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kenneth Komba kutoka Idara ya Elimu mkoa wa Iringa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Spring Valley iliyopo Mkoani Iringa.

Alisema kuwa mtoto wa kike akipatiwa elimu kuna uwezekano mkubwa kwa taifa kuwa na maendeleo kutokana na kuwajibika kwao katika maisha ya kila siku hivyo wazazi na walezi ni muhimu kuwasomesha watoto wa kike kwa lengo la kuendeleza ndoto walizonazo.

Alisema kuwa jukumu la kusomesha elimu ya msingi hadi sekondari ni la serikali lakini wazazi na walezi wanaosomesha shuleni hapo ni kuisaidia serikali hivyo ipo tayari kupokea changomoto zote katika shule hiyo na kushirikiana kuzitatua.

Komba aliipongeza shule ya sekondari Spring Valley kwa kuwa moja ya shule zinazofanya vizuri mkoani hapa kielimu na tabia kwani ni moja ya shule ambazo idara ya elimu haipati malalamiko ya mara kwa mara kutoka shuleni hapo.
 Wanafunzi wa shule ya wasichana ya Spring valley wakicheza muziki katika sherehe za kumaliza kidato cha nne
 wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Springa Valley wakiwa katika picha ya pamoja
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Spring Valley iliyoko katika manispaa ya Iringa wakiwa katika mafunzo ya vitendo shuleni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...