Takribani raia 800 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamekimbilia Nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi katika kijiji cha Kigadye Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma wakihofia machafuko. 

Raia hao ambao wengi wao wanatoka maeneo ya Fizi na misisi Kivu kusini mwa Congo wamedai kuwa Vikosi na wapiganaji wa maimai nchi Congo na vikundi mbalimbali vya waasi vinavyoendelea kupigana nchini vimewatia hofu na hivyo kuanza kukimbia nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi.

Wakizungumza mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma iliyotembelea katika kituo cha kupokelea waomba hifadhi kijiji cha Kigadye raia hao walisema sababu iliyowafanya kukimbilia Tanzania ni hofu ya usalama wa maisha yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikundi vya waasi na Serikali iliyopo madarakani.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (mst.) Emannuel Maganga akiongoza kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa amesema tayari Mkoa umefika kuwaona raia hao na wanafana jitihada za kuhakikishah wanapatiwa huduma muimu za kibinadamu zinaboresha katika eneo hilo wakati kamati ya taifa ya kusikiliza maombi ya ukimbizi inajiadaa kuwasikiiza raia hao.

Kutokakana na wimbi kubwa hilo huduma za kibinadamu ikiwemo chakula, malazi zinahitajika haraka ili kuwahudumia raia hao ambao wengi wao ni kinamama na watoto. Baadhi ya raia waliokimbilia nchini Tanzaia wamedai kuwa kutokana na kuahirishwa Uchaguzi Mkuu uliopaswa kufanika Desemba, 2017 dalili za kuzuka kwa mzozo wa mapigano uenda ukawaathiri amani nchini Congowa, Vyama vya upinzanu vimeanza kuonesha dalili za kupinga kusitishwa kwa uchaguzi, wamehofia amani.

Kituo cha kigadye wilayani kasulu, huenda kikashindwa kimili idadi kubwa ya raia wa Congo wanaoendelea kfika kituoni hapo kwa madai ya kukimbia vita nchini mwao. Kusini mwa Congo kumekuwa na matukio ya hivi karibuni mashambulio ya mara kwa mara yanayosabisha hofu ya machafuko kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. Emannuel Maganga (mwenye kofia) akikagua makazi ya raia waomba hifadhi kutoka Congo DRC katika kituo cha Kigadye Wilayani Kasulu. 
Baadhi ya raia kutoka Jamuri ya Kidemokrasia ya Congo DCR wakifuatilia ujio wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigomailipowasili kukagua kituo cha Kigadye Wilayani Kasulu. 
Mmoja wa waomba hifadhi akieleza mbele ya Kamati ya Ulinzi ya Mkoa sababu zilizo wafanya wakimbilie Tanzania
Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR Kigoma(mwenye kofia ya bluu) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma hali ya kituo cha kupokelea Wakimbizi Kigadye.Habari na Picha zimeandaliwa na.Gabriel Ng’honoli Afisa Habari,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...