Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye Makao yake makuu jijini Arusha inafanya ziara ya kikazi katika Jamhuri ya Cape Verde ili kukutana na kuelimisha wadau mbalimbali nchini humo kwa lengo la kuiitangaza Mahakama hiyo.

Uelimishaji huo ni miongoni mwa juhudi zinazofanyika na Mahakama hiyo ili kuongeza uelewa wa wadau husika kuhusu jukumu na ujumbe wa AFCHPR katika suala zima la kulinda haki za Binadamu baranni Afrika na pia kuzihimiza nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuridhia itifaki iliyounda Mahakama hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 34(6) na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali Mamlaka ya AfCHPR kupokea kesi za Watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali.

Katika ziara hiyo ya siku tatu inayoanza leo,13/12/2017 Jumatano wajumbe wake ambao ni pamoja na Majaji watatu na baadhi ya maofisa wa ofisi ya Msajili wa Mahakama hiyo watakutana na Rais wa Cape Verde,Waziri mkuu na Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo na wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria na wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali.

Rais wa Mahakama hiyo ya Afrika ya haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Ore’ alisema ziara hiyo ya uelemishaji kuhusu Mahakama hiyo ni wan ne kufanyika kwa mwaka huu na kwamba juhudi hizo zitaendelea mwaka ujao wa 2018.

“Ili kufanikisha malengo ya AfCHPR na pia kuimarisha mfumo wa Haki za Binadamu barani Afrika nchi za umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa mujibu wa kifungu husika” alisema Jaji Ore’.

Tayari kwa mwaka huu uelimishaji huo umefnayika katika nchi za Jamhuri ya kiarabu ya Misri,Tunisia na Guinea Bissau.

Aidha hadi sasa ni nchi 30 tu kati ya 55 wanachama wa umoja wa Afrika ikiwemo Tanzania ndiyo zimeridhia itifaki iliyoanzisha AfCHPR na kati ya hizo ni nchi 8 tu ndiyo zimekwisha toa tamko la kuitambua Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...