Balozi wa Kuwait nchini ,Mhe.Jasem Al- Najem akizungumza na baadhi ya wananchi wa Vigwaza kwenye zahanati ya Vigwaza Chalinze Bagamoyo Mkoani Pwani baada ya kumkabidhi diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani vifaa vya watu wenye ulemavu na mabeseni 100 yenye vifaa vya uzazi vyote vikiwa na thamani ya mil.17.5.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Balozi wa Kuwait nchini ,Mhe.Jasem Al- Najem wa kwanza kushoto akikabidhi vifaa vya watu wenye ulemavu na mabeseni 100 yenye vifaa vya uzazi vyote vikiwa na thamani ya mil.17.5, Kwa diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani wa pili kutoka kulia.

Na Mwamvua Mwinyi,Vigwaza.

Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jasem Al- Najem amemkabidhi diwani wa kata ya Vigwaza, jimbo la Chalinze Bagamoyo mkoani Pwani, Mohsin Bharwani vifaa vya watu wenye ulemavu na mabeseni 100 yenye vifaa vya uzazi vyote vikiwa na thamani ya mil.17.5. Kati ya fedha hiyo kiasi cha sh. mil 13 ni gharama ya vifaa vya watu wenye ulemavu ikiwemo magongo 20, fimbo za wenye ulemavu 10, fimbo za walemavu wa macho 10, miwani 20, mafuta ya wenye ulemavu wa ngozi na viti vya kubebea wagonjwa kwa watu wazima 20 na kwa watoto kumi.

Pamoja na hilo, sh mil 4.5 ni gharama ya mabeseni 100 yenye vifaa vya akinamama wajawazito kabla na baada ya kujifungua. Akipokea vifaa hivyo, kwenye zahanati ya Vigwaza, diwani wa kata ya Vigwaza Bharwani alimshukuru balozi wa Kuwait nchini Al-Najem na kusema ni balozi wa mfano na anastahili kuigwa.

Alieleza wamekuwa wakishuhudia misaada mingi ikielekezwa mijini lakini balozi huyo amefika kijijini kwa watu wenye shida na wanaohitaji misaada kama hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...