Mkuu wa kitengo cha masoko cha Exim Bank Tanzania, Stanley Kafu pamoja na wafanyakazi wa tawi la Arusha wakikabidhi vitanda na magodoro 40 kwa mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dk Timothy Wonanji.

HOSPITALI na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Kama sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii, Benki ya Exim Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya mkoa ya Mount meru iliyoko Arusha.

Hospitali ya mkoa ya Mount Meru, Arusha, ni hospitali ya tano kupokea mchango huu, baada ya Hospitali ya rufaa Dodoma mwezi uliopita, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka huu. Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo na mgeni rasmi alikwa Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa, Arusha Dr Vivian Wonanji.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu alisema, “ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini. Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.” 

Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa Arusha Dr. Vivian Wonanji alipongeza Exim Bank Tanzania kwa ahadi yake ya kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye ma hospitali ambao unakabiliwa na taifa na kuleta juhudi zake kwa hospitali ya mkoa ya Arusha. Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa, Mount Meru alisema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii.”
Ikiwa kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Mtwara, Pemba na Unguja ambapo mpaka sasa Dar es Salaam, Unguja, Mtwara, na Dodoma tayari wameshapokea misaada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...