Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewaagiza wahandisi wa ujenzi katika Halmashauri zote hapa nchini kuona uwezekano wa kutumia Tiles badala ya kuweka sakafu ya kawaida ili kuongeza uimara na mandhari majengo hayo.

Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa na mabweni ya shule ya sekondari Hamza na miundombinu mbalimbali ya kituo cha afya cha zogolo yakiwepo majengo ya upasuaji, maabara, na wodi ambapo majengo yote ameyakuta yamejengwa vizuri sana kwa kuwekwa Tiles. 

Ameeleza kwamba majengo mengi yanayojengwa na kuwekwa floor(sakafu) ya kawaida yanabomoka kwa muda mfupi na hivyo kuhitajika kufanyiwa ukarabati mara kwa mara.Waziri Jafo amesisitiza kwamba ujenzi wa kutumia Tiles kusaidia hata katika usafi wa majengo hayo. 

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amewapongeza viongozi wa wilaya ya Nzega wakiwemo wabunge wao Hussein Bashe, Selemani Zedi, na Hamisi Kigwangwala kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi wao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Viongozi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wakipata maelekezo ya matumizi ya Tiles kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wakielekea kwenye kukagua jengo jipya la upasuaji katika Kituo cha Afya cha Zogolo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...