Uongozi wa serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania inayoongozwa na Dr. John Pombe
Magufuli ni mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika kwa kuwa umekuwa makini kutumia
vizuri rasilimali za nchi kwa manufaa ya watu wake.
Viongozi wengi wa kiafrika
wamekuwa wakitumia vibaya rasilimali za nchi zao kwa kujilimbikizia mali huku
wananchi wakibaki kuwa masikini wa kutupa. Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa
Dr. Magufuli unapambana na wanaofuja mali za uma pamoja na kuepuka sherehe na
mikutano isiyo ya lazima ili kuokoa pesa kwa ajili ya kuendesha miradi ya maendeleo.
Hayo yalisemwa na Rev. Dr. Celestino Chishimba alipokuwa akiongoza sala maalumu ya
kuadhimisha uhuru wa Tanzania iliyofanyika jumapili iliyopita kwenye kanisa la Anglican
Holy Cross Cathedral jijini Gaborone nchini Botswana.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na baadhi
ya watanzania waishio nchini Botswana wakiongozwa na viongozi wa chama cha
watanzania chini Botswana. Viongozi waliohudhuria ni Mwenyekiti, Bw. Nieman Kissasi,
Makamu Mwenyekiti Bi Rehema Mselle Kalabamu, Katibu Bi Magret Tibesigwa na
Mweka fedha Msaidizi Bi Haika Marandu. Historia fupi ya Tanzania ilitolewa na Eng. Ben
Rugumyamheto.
Sherehe za kuadhimisha uhuru wa Tanzania zilihitimishwa na hafla iliyoandaliwa na
Chama cha Watanzania nchini Botswana (ATB). Hafla hii ilifanyika kwenye kumbi za
mikutano za Maharaja Gaborone juzi jumamosi. Mgeni rasmi kwenye hafla hii alikuwa
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini anayehudumu pia Botswana, Mh. Silvester Ambokile.
Wageni wengine waliohudhuria sherehe hizi ni pamoja na Bw. Richard Lupembe kutoka
ubalozi wa Tanzania uliopo Pretoria Afrika Kusini na mwenyekiti wa Chama cha
Waganda nchini Botswana Bw. Jonathan Beesigomwe aliyeuwakilisha umoja wa wana
Africa Mashariki nchini Botswana.
Mh. Balozi aliwapongeza wana jumuia ya watanzania
nchini Botswana kwa kudumisha umoja na ushirikiano miongoni mwao kwani ni mfano
wa kuigwa kusini mwa Afrika. Aliwasihi watanzania kukumbuka kuwekeza nyumbani
Tanzania hasa wakati huu ambapo nchi yetu inahamasisha uwekezaji kwenye kilimo,
elimu na viwanda.
Waumini waliohudhuria ibada maalumu ya kuiombea Tanzani wakimsikilisha
Padre Chishimba alipokuwa akielezea kuhusu uongozi wa Tanzania wakati alipokuwa
akihubiri.
Baadhi ya watanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania.
Padre Dr. Chishimba na Bw. Kissasi wakikata keki maalumu iliyoandaliwa ya
kuadhimisha uhuru wa Tanzania. Wanaoshuhidia zoezi hilo ni Bi Rehema kalamabu na
Eng. Ben Rugumyamheto
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini anayehudumu pia Botswana, Mh. Silvester Ambokile akiwahutubia watanzania waliohuduria hafla
ya kuadhimisha uhuru juzi jumamosi kwenye kumbi za Maharaja jijini Gaborone.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...