THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAKALA SHERIA:KUBADILI HATI KUTOKA JINA LA MAREHEMU KWENDA MSIMAMIZI WA MIRATHI.

Na  Bashir  Yakub.

Mara  kadhaa nimezungumzia   kuhusu  namna  bora  na  ya  kisheria  ya  kuuza  na  kununua  nyumba  au  kiwanja    kutoka  kwa msimamizi  wa  mirathi  baada  ya   mmiliki  halisi  kufariki.

Leo  tena makala haya yataeleza  kubadili  jina kutoka  jina  la  marehemu  kwenda  kwa  msimamizi  wa  mirathi. Kubadili  huku  kunaweza  kuwa  na  lengo  la  kuuza, kupangisha  , kugawa  kwa  warithi  au  hata  kubadili tu  kwa maana  ya  kubadili  bila  malengo haya juu.

Maelezo  katika  makala  haya yatatoka Sheria  ya  Usajili  wa  Ardhi  sura  ya 334 na  kanuni zake  za  mwaka  1954, pamoja  na Sheria ya  usimamizi  wa  Mirathi sura ya 352 na  kanuni zake  za mwaka 1963.

UTARATIBU  NI  HUU.

1.Lazima  kwanza ufungue  mirathi na  apatikane  msimamizi  wa  mirathi.  Tumeeleza  mara  nyingi utaratibu  wa  kufungua  mirathi . Tulisema kuwa,  kwa  marehemu  aliyekuwa  mkristo  utafungua  mahakama  maalum ya  wilaya(district delegate)  au mahakama kuu  ,  na  kwa  marehemu  aliyekuwa  muislam  au  aliyeishi  kimila  bila  dini   utafungua  mahakama  ya  mwanzo  au  Mahakama  kuu.
Kwahiyo hoja  hapa  ni  kuwa  hatua  ya  kwanza   lazima  awepo  msimamizi wa mirathi.
2. Msimamizi wa  mirathi  atakapokuwa  amepatikana  basi  atapewa  fomu  namba 4 na 5 za  usimamizi  wa mirathi. Fomu  hizi  zinatolewa  na  mahakama  na  ni  uthibitisho  kuwa   fulani  ni  msimamizi  wa  mirathi halali.  Hoja hapa hakikisha  unazo hizo  fomu   mkononi.
3. Ukishakuwa  na  fomu  hizo  mkononi  basi  utatakiwa  kutafuta  na  kujaza  fomu  nyingine iitwayo  fomu  ya  uwakilishi  maalum  wa  marehemu kisheria( Lega personal representative). Fomu  hii  ni  namba 20  kwenye  kanuni  za  usajili wa ardhi.

                KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com