NA IS-HAKA OMAR, DODOMA.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, Gaudencia Kabaka amewataka wanawake wa umoja huo kuvunja makundi ya ngazi zote yaliyojengeka wakati wa uchaguzi na badala yake wafanye kazi za kuwatumikia kwa ufanisi wapiga kura waliowapa ridhaa ya kuongoza.

Pia, amesema UWT kupitia uongozi wake mpya ulioingia kwa sasa ni lazima irejeshe heshima yake ya kuwa chombo cha kuwaunganisha wanawake wote wa mijini na vijijini Tanzania ili wapate maendeleo.Wito huo ameutoa katika hafla ya mapokezi ya uongozi huo yalioandaliwa na UWT Mkoa wa Dodoma katika viwanja vya White house Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Amesema bila kuvunja makundi Umoja huo hautopata maendeleo na watatumia muda mwingi kulaumiana, kuangaishana na hamaye kukosa muelekeo wa kutekeleza ahadi walizotoa kwa mamilioni ya wanawake wa Tanzania.Kabaka ameeleza kwamba Umoja wa Wanawake Tanzania ni chombo cha CCM kinachotakiwa kuwa nguzo na muhimili mkuu katika kusimamia na kulinda maslahi ya Chama kisiasa, kiuchumi na kijamii.

"Furaha yangu ni kwamba mlituchagua kihalali bila ya kutumia rushwa, hivyo nasi tuna deni la kuwalipa ambalo ni lazima tutimize utumishi bora na uliotukuka kwa miaka mitano ya uongozi wetu.Na nakuombeni tushirikiane kwa pamoja kupinga rushwa na ufisadi ndani ya UWT na Chama kwa ujumla kama tunavyopinga makundi ya kuhatarisha uhai wa Chama cha Mapinduzi", amesema Mama Kabaka.
VIONGOZI Mbali mbali wa UWT walioudhuria katika hafla ya mapokezi ya viongozi wapya UWT ngazi ya Taifa.
MWENYEKITI wa UWT Taifa, Gaudencia Kabaka akihutubia katika hafla ya mapokezi ya viongozi wapya ngazi ya Taifa wa Umoja huo yaliyofanyika katika viwanja vya White House Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...