Naibu Waziri Mhe. Injinia Stella Manyanya afungua rasmi mkutano kwa njia ya Mtandao yaan (Video Conference) wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Mamlaka za mikoa na Halmashsauri za Wilaya kuhusu masuala ya sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na taasisi zake leo Tarehe 18 – 20 Disemba, 2017 na kuunganisha wadau kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe, Kilimanjaro, Ruvuma, Kigoma, Lindi, Singida, Pwani na Dodoma.

Mhe. Naibu Waziri aliwashukuru Makatibu Tawala wa Mikoa, Wasaidizi wao na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya ambao wameitikia wito pamoja na wataalamu na maafisa mbalimbali.

Wizara ilianza na taasisi yake ya BRELA ambayo ilielezea majukujumu yake na huduma mbalimbali wanazotoa kwa umma na kutoa fursa ya wadau kutoka mikoa yote iliyoshiriki walipata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...