Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli amewataka wanachama wa CCM kuchagua viongozi bila kuangalia maslahi urafiki, dini, kabila kadhalika amewasihi kutochagua viongozi watoa rushwa kwa kusema kuwa rushwa ni adui wa haki.
Amesema kiongozi anapaswa kuwa mfano kwa wanachama na wananchi. Hapaswi kutuhumiwa kwa sifa mbaya kama ujambazi, madawa ya kulevya, rushwa n.k. Kuna msemo maarufu unasema 'mke wa Mfalme hapaswi kutuhumiwa kwa kuchepuka'
"Sio siri kuwa mageuzi tuliyoyafanya ni makubwa sana na hatuna budi kuyasimaia na viongozi waliochaguliwa ndio watakakuwa na majukumu hayo"  Alisema  Rais Magufuli
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk.John Magufuli akizungumza na wanachama wa chama cha Mapinduzi wakati akifungua kifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo Jumatatu Desemba 18, 2017.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...