THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

SERIKALI IMETUMIA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 500 KUKAMILISHA MRADI MKUBWA WA UMEME WA KV 400 KUTOKA IRINGA HADI SHINYANGA

Na Jumbe Ismailly 
SERIKALI imetumia zaidi ya shilingi bilioni 500 kugharamia mradi wa usambazaji wa nishati ya umeme wa msongo wa KV 400 ulioanza kutekelezwa mwaka 2016 na kukamilika mwaka 2016  kutoka Mkoani Iringa kupitia Dodoma, Singida, Tabora hadi mkoani Shinyaga.

Meneja Njia kuu za umeme, Amosi Kaihula alisema kiasi hicho kikubwa cha fedha kilichotumika kusambaza miundombinu hiyo ya nishati ya umeme, haina budi kuhakikisha inalindwa na kila mwananchi na inakuwa salama kwa wakati wote ili huduma hiyo iweze kuendelea kupatikana.

Aidha meneja huyo aliweka bayana kwamba kwa hiyo inapotokea mhalifu mmoja anapokwenda kuchukua na kuangusha nguzo ulipopita umeme huo wa msongo wa taifa na kuanguka chini, serikali huingia hasara kubwa sana na kwamba idadi kubwa ya wananchi hukosa huduma hiyo ya umeme.

Kwa mujibu wa Kaihula gridi ya taifa imeungana na kwa hali hiyo endapo njia moja itaanguka na kuchangia kukosekana kwa umeme, itasababisha pia mikoa yote iliyoungamishwa katika gridi ya taiafa kukosa pia huduma hiyo ya umeme pia.
 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Emmanueli Luhahula akitoa maelezo ya jitihada zinazofanywa na wilaya hiyo kwa kushirikiana na TANESCO kukabiliana na wizi pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umeme katika wilaya hiyo.
 Afisa usalama wa TANESCO Mkoa wa Singida,John Chilali (wa kwanza kutoka kushoto) akibadilishana mawazo nje ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Iramba na afisa mahusiano wa shirika hilo Mkoani Singida, Witness Msumba (wa pili kutoka kushoto). 
 Meneja Njia kuu za umeme, Amosi Kaihula akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari juu ya fedha zilizotumika kukamilisha mradi huo mkubwa wa KV400 na mikakati ya kukabiliana na wizi pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umeme katika njia kuu ya kusambazia nishati hiyo.
Nyaya za kusambazia umeme katika njia kuu ya kutoka Mkoa wa Iringa hadi Shinyanga yenye msongo wa KV400(Picha zote Na Jumbe Ismailly)