Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini
(DCEA) imesema ipo mbioni kutoa mwongozo wa kuratibu na kusimamia
viwango vinavyowiana vinavyotarajiwa kutumika katika Vituo vyote vya
Upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya nchini.
Hayo
yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mashirika yasiyo ya
Serikali NGO’s kutoka (DCEA), Salome Mbonile wakati wa sherehe za
maadhimisho ya miaka minne ya kituo cha upataji nafuu kwa watumiaji wa
dawa za kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mbonile
alisema katika kuhakikisha kuwa mwongozo huo unaleta tija
iliyokusudiwa, Serikali inatarajia kuwashirikisha wadau wote katika
mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ili waweze kutoa mapendekezo,
ushauri na maoni ili kuweza kuisaidia jamii hususani makundi ya vijana
katika kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya.
"Kumekuwa
na uwoga kwa wananjamii kutembelea Sober House (Nyumba za upataji nafuu
kwa watumiaji wa madawa ya kulevya, lakini kupitia mwongozo huu
tunataka kuweza viwango vinavyofanana ili kutoa fursa kwa watu wote
kutembelea makazi haya" alisema Mbonile.
Mbonile
alisema mapambano ya vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya nchini
hayana budi kuungwa mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo na hivyo
Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa na asasi, taasisi mbalimbali
ili kuhakikisha kuwa jamii ya Kitanzania hususani vijana inaendelea kuwa
salama na kuondokana na matumizi ya dawa za kuelvya.
Aliongeza
kuwa hadi sasa Tanzania ina jumla ya Nyumba za upataji nafuu kwa
watumiaji wa dawa za kulevya 25 pamoja na Asasi 16 zinazotoa elimu na
kuhamasisha jamii kutambua madhara mbalimbali yatokanayo na matumizi ya
dawa za kulevya ikiwemo hatari ya maambuzi ya magonjwa mbalimbali pamoja
na vifo.
Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Upataji nafuu kwa watumiaji wa Dawa za Kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Upataji nafuu kwa watumiaji wa Dawa za Kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand na Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali(NGO's) kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile (katikati).
Mmoja wa wanufaika wa Kituo cha upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam Bi. Amina Mbonde akitoa ushuhuda namna alivyofanikiwa kuacha matumizi ya dawa za kulevya wakati wa hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa kwa kituo hicho jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed, Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand na Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile na Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...