Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, imezindua kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Makamu Mwenyekiti wa TYPF Training Centre, Saida Babde alisema ndoto yao ni Taasisi yao kuwa dira ya mtoto wa kike nchini Tanzania kwa namna moja ama nyingine, huku uzinduzi huo ukihudhuliwa na watu mbalimbali akiwamo Mbunge wa Viti Maalum Zainabu Vullu na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mheshimiwa Naseem Al Najim.

"Ndoto yetu ni kumkomboa mtoto wa kike kwa kupitia kituo chetu ambacho kitakuwa kinafundisha mambo mbalimbali kama charahani, kompyuta na kazi nyingine za mikono.

"Nawaomba Watanzania kuchangamkia fursa hii ambapo tumeanzisha ndani ya uwapo wa Taasisi yetu ya TYPF, ambapo sote kwa pamoja tuna kiu ya kumkwamua Mtanzania,"Alisema.

Naye Mheshimiwa Zainabu, Mbunge wa Viti Maalum aliwashukuru TYPF kwa kuguswa na mambo ya kijamii, hususan dhamira ya kumkwamua na kumsaidia mtoto wa kike bila kusahau wale wanaoishi kwenye mazingira magumu.
 Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem(wa pili kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya DHE Nureiyne ya Iringa, Sheikh Said Bin Abri.
 Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF, Ally Bakry akitoa historia fupi ya uanzishwaji wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF wakati wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi uliofanyika kituoni hapo Upanga jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa  uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre pamoja na kuomba uongozi wa taasisi hiyo kujikita zaidi kwa wasichana walioko pembezoni mwa mkoa wa Dar Es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem akizungumza jambo wakati wa  uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
 Kaimu wa taasisi isiyo Serikali ya TYPF, Saida Babde akitoa ufafanuzi wa uendeshwaji wa kituo hicho na kazi zitakazofanyika kituoni hapo wakati wa uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
 Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya DYCCC, Hassan Akrabi(kushoto) akimkabidhi cheti cha heshima kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem(kulia) kwa mchango waliounesha wakati wa uanzishwaji wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.
 Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum, Zaynabu Matitu Vulu, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem pamoja na Mkuu wa taasisi isiyo Serikali ya DHE Nureiyne ya Iringa, Sheikh Said Bin Abri wakiwa wamekaa kwenye viti wakitumia Tarakilishi mpakato (laptop computer) wakati wa  uzinduzi wa kituo cha Ufundi kinachojulikana kama TYPF Training Centre, Upanga kwa nia ya kuendeleza watoto wa kike katika mambo mbalimbali ya kimaisha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...