Shirika la Umeme Nchini TANESCO, limesema kuwa linaendelea kuimarisha Mifumo na Miundombinu ya Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji umeme, lengo kuu kwa sasa likiwa ni Kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa Uhakika na unaokidhi mahitaji ya kijamii na kimaendeleo kwa Wananchi ,wajasiriamali na wawekezaji mbalimbali wakiwemo wale wakubwa wa kati na hata wale wadogo

Hayo yamesemwa na Meneja mwandamizi Usambazaji Umeme wa TANESCO Mhandisi Raymond Sweya wakati wa Maonesho ya Pili ya ya bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Mw. J k. Nyerere Sabasaba Jijini Dar es salaam

''Tunaendelea kuimarisha na kupanua mifumo yetu ya usafirishaji na usambazji umeme pamoja na ile ya uzalishaji umeme ili kuhakikisha kuwa Sekta hii ndogo ya Nishati ya umeme inazidi kuimarika kwa kuwahudumia wateja wetu kwa huduma bora za umeme na zinazokidhi mahitaji'' alisema Mhandisi Sweya

Aliongeza kuwa mbali na utoaji wa huduma za umeme wa uhakika lakini TANESCO imedhamiria kutoa huduma hizo kwa bei nafuu itakayowezesha kupunguza gharama za uzalishaji na hivyo kuwezesha hata punguzo bei ya bidhaa husika na zitakazoweza kukidhi ushindani wa kibiashara katika soko la ndani na nje ya Nchi

Katika maonesho hayo yalishoshirikisha washiriki zaidi ya 500, TANESCO ilishiriki kama mdau Muhimu na wa karibu katika uendelezaji wa sekta nzima ya ujenzi na uendelezaji wa viwanda Nchini. 

Uwepo wa Umeme wa kutosha Nchini ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kuvutia uwekezaji mkubwa, mdogo na wa kati katika sekta nzima ya Viwanda Nchini na hvyo kuongeza ustawi wa maendeleo ya Kijamii  na kiuchumi kwa kutoa ajira, kukuza Soko la bidhaa za ndani, mauzo ya nje ya nchi pamoja na Kukuza uchumi wa Nchi nzima kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...