Wananchi Wilayani Igunga mkoani Tabora Wametakiwa Kujenga Tabia na mazoea ya Kutunza miundombinu ya Umeme, kwani kwa Kufanya hivyo kutaifanya Tanzania kuwa nchi yenye Uchumi wa Kati Kupitia Sekta ya Viwanda kutokana na Umeme wa Uhakika.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Tabora na Meneja wa Njia kuu za Umeme, Mhandisi Amos Kaihula, ambapo amesema ni Jukumu la Wananchi Kwenye maeneo yao Kuhakikisha kwamba Miundo mbinu ya Umeme inakuwa Salama wakati wote.

Sambamba na wito huo, Mhandisi Kaihula amewaasa wananchi kukemea kwa nguvu viashiria na Matukio yenye mrengo wa Kuhujumu Miundombinu ya Umeme." Mtu mmoja mwenye dhamira mbaya anaweza kuleta hasara kubwa kwa jamii yote na nchi nzima pale hujuma na wizi wa vyuma unapofanyika katika njia kuu ya umeme na kupelekea nguzo kubwa ya grid ya taifa kuanguka" alisema Mhandisi Kaihula.

“Ndugu zangu, miundombinu hii ya Umeme mnayoiona, imetengenezwa kwa gharama na jitihada kubwa mno za serikali, lakini inapotokea mtu amejaribu kuisogelea miundombinu hiyo, madhara yake ni makubwa ikitokea lile tower (muundo mbinu) limeanguka, umeme wake ni mkubwa mno, na inaweza kuleta maafa makubwa na athari kubwa kwa nchi kiuchumi na kiusalama” aliongezea mhandisi Kaihula.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Igunga Robert Mwagala amekemea vitendo hivyo vya Uhujumu wa miundombinu ya umeme, na kusema Serikali ikishirikiana na TANESCO itafanya zoezi la kubaini wahujumu hao, na watachukuliwa hatua za kisheria.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Igunga Robert Mwagala akizungumza na Wananchi wa Kata hiyo wakati wa Kampeni ya Utoaji Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Kulinda Miundombinu ya Umeme ya Tanesco, katika Kijiji cha Mgongolwa Wilayani Igunga mkoani Tabora.

Wakazi wa Kijiji cha Mgongolwa wakisikiliza kwa umakini elimu iliyokuwa ikitolewa na Maofisa wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, kuhusiana na umuhimu wa Kulinda miundombinu ya Shirika hilo.
Baadhi ya miundombinu ya njia kuu ya umeme za Msongo wa Kilovolti 220 na Kilovolti 400 zinazopita katika mikoa ya Singida na Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...