Leo Ijumaa, 15 Desemba 2017, Benki ya TPB tumeendelea kusogeza huduma zetu karibu zaidi na wateja kwa kufungua tawi jipya maeneo ya Kwa Mrombo, Mkoani Arusha.

Lengo la kufungua tawi hili ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na pia kupata fursa ya kutoa huduma kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi, ili wakazi wa mkoa wa Arusha, hususan waishio maeneo ya Kwa Mrombo, waendelea kufaidika na huduma bora zenye gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa kuzindua tawi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya alisema tawi hilo jipya litaongeza idadi ya wateja kwenye benki hiyo.

Alisema pia wakazi wa Kwa Mrombo, watafaidika na mikopo mbalimbali inayotolewa na TPB inayokidhi mahitaji ya vikundi, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, mikopo ya wafanyakazi na hata wastaafu.

‘Ni furaha kubwa sana kwetu sisi TPB kuweza kufikisha huduma zetu hapa Kwa Mrombo. Ni matumaini yangu kuwa tawi hili litaongeza idadi ya wateja watakaofika kupata huduma mbalimbali tunazozitoa, kwani TPB tunatoa huduma bora na zenye kukidhi matakwa ya kila mwananchi katika jamii ikiwemo mikopo kwa vikundi visivyo rasmi,’ alisema Profesa Rutashobya.

Alisema kwa sasa lengo lao kubwa ni kuendelea kutoa huduma bora zaidi ili kuwanufaisha wananchi wa kipato cha chini. ‘TPB inaendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi kwani mbali na kufungua tawi hili, katika kipindi cha mwaka huu tumeweza kufungua matawi yetu huko Mwanjelwa Mkoani Mbeya, Mto wa Mbu wilayani Monduli na Temeke,’ alisema.

Kwa upande wake, Meneja wa tawi la Kwa Mrombo Hussein Jalala alisema mwitikio wa wakazi wa maeneo ya Kwa Mrombo umekuwa mzuri, tangu walipoanza kutoa huduma zake maeneo hayo. Alisema tawi lake limejipanga vizuri kuhakikisha kuwa huduma zitakazotolewa kwa wateja wao ziwe za kuridhisha na zenye kukidhi mahitaji yao. Jalala alizitaka taasisi mbalimbali vikiwemo vyuo, mashirika na hata shule kufungua akaunti za taasisi na TPB ili kupata huduma za kisasa na zenye gharama nafuu. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobya akifurahia  baada ya kufungua rasmi tawi jipya la benki hiyo maeneo ya  kwa Mrombo ,huko Mkoani Arusha. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi .
Mwenyekiti wa Bodi ya Waurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa, akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw. Tate Looboye Koole, wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya  Kwa Mrombo, Mkoani Arusha. Katikati ni Meneja wa tawi hilo Hussein Jalala.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa (wa pili kushoto), akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo Bw. Elias John Malisa, wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya  Kwa Mrombo, Mkoani Arusha. Kushoto  ni Meneja wa tawi hilo Hussein Jalala na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo pamoja na baadhi ya wakurugenzi, kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo lililopo maeneo ya kwa Mrombo, Mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Prof. Lettice Rutashobwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa tawi la benki hiyo lililopo maeneo ya kwa Mrombo, Mkoani Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...