CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewataka viongozi wake wote waliochaguliwa hivi karibuni katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanawatumikia wanachama na wasio wanachama kwa uadilifu na uzalendo ili kuendelea kukijengea imani Chama hicho kwa watu wote. 

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Nzega na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati anakabidhi vitendea kazi (pikipiki 19) kwa viongozi na watendaji wa Chama hicho katika Jimbo la Nzega vijijini vilivyotolewa na Mbunge wao na kuweka jiwe la Msingi kwenye Kitega Uchumi CCM wilaya ya Nzega.
Alisema kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kwa viongozi wapya walichaguliwa kuwatumikia wanachama wote waliowachagua na ambao hawakuwachagua ili kuendelea kukiimarisha Chama chao. 

Kinana alisema kuwa uchaguzi umekwisha kinachofuata ni kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 hadi 2020, ahadi za Mgombe wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizitoa wakati akiomba kura na zile zilizotolewa na Wabunge ambazo hakuwa katika Ilani. Alisema kuwa ni muhimu kwa MwanaCCM na watumishi wa umma na wananchi wengine kuhakikisha wanatekeleza Ilani ya Chama hicho ambacho kiko madarakani. 

Aidha Kinana aliwataka viongozi na watendaji waliopatiwa vifaa hivyo kuvitumia kwa ajili ya shughuli za kukiimarisha zaidi Chama na sio kwa ajili ya mambo mengi ambayo sio malengo yake. 

Naye Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala alisema kuwa uchanguzi umekwisha ni vema wakawa wamoja kwa ajili ya kuendelea kujenga Chama chao. 

Alisema kuwa ataendelea kushirikiana na wanachama wote walioshinda na walioshindwa kwa ajili ya kuimarisha mshikamano ndani ya CCM na kwa ajili kuendelea kukipa matokeo mazuri katika chaguzi mbalimbali zijazo. 
Dkt. Kigwangala alisema kuwa pikipiki 19 ni za CCM na sio ya watu waliokabidhiwa na hivyo viongozi na watendaji wa Chama waliopata wanatakiwa kuzitumia katika kuimarisha Chama hicho kwenye maeneo yao ya kazi. Alisema kuwa Jimbo la Nzega Vijiji ni kubwa kwa hiyo usafiri huo utawasaidia kuwafikia wanachama na watu wengi na hivyo kukijenga Chama hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...