Wakaguzi wa Migodi Nchini wameagizwa kutembelea mara kwa mara kwenye migodi hususan ya wachimbaji wadogo kwa ajili ya kukagua hali ya usalama na kuwasaidia Wachimbaji kuepusha ajali wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.

Agizo hilo limetolewa Desemba 14, 2017 Mkoani Tabora na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alipotembelea kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilaya ya Kaliua ili kujionea shughuli zinazofanywa mgodini hapo na kuzungumza na wachimbaji.

Baadhi ya Wachimbaji walimueleza Naibu Waziri Nyongo kuwa wamekuwa wakifanya shughuli zao katika mazingira magumu bila kuwa na elimu ya namna bora ya uchimbaji wa madini.

Nyongo alisema ni jukumu la Maafisa Madini wakiwemo Wakaguzi wa Migodi (Mining Inspectors) kuhakikisha wachimbaji hususan wadogo wanapatiwa elimu ya mara kwa mara kuhusu afya, uchimbaji salama na uhifadhi wa mazingira ili kuepusha magonjwa na ajali zinazosababishwa na uelewa finyu wa uchimbaji bora.

“Wachimbaji wadogo wanapaswa kutembelewa na kuelimishwa mara kwa mara na hili ni jukumu lenu, msisubiri hadi kutokee madhara ndio mfike kutoa elimu,” alisema.Aidha, Nyongo aliagiza wamiliki wa machimbo kuhakikisha wanawapatia vitendea kazi wachimbaji kwenye maeneo yao ili kuwalinda na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza kwenye mkutano na Wananchi na Wachimbaji Wadogo kutoka Kata ya Silambo Wilayani Kaliua (hawapo pichani).
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akielekea kwenye machimbo ya dhahabu yaliyopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kutoka kulia) akitazama moja ya shimo la dhahabu lililoko katika Mgodi wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele) akiongoza ujumbe wake kukagua shughuli za uchimbaji wa dhahabu kwenye mgodi wa dhahabu wa Nsungwa Gold Mine uliopo katika Kata ya Silambo Wilayani Kaliua.

HABARI ZAID BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...