Zantel kwa kushirikiana na Bodi ya Mamlaka ya Mapato ya Zanzibar wameingia katika makubaliano ambayo yatawawezesha wakazi wa kisiwani hapa kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa inayotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel.

Ushirikiano huo unawezesha wateja wote wa Bodi ya Mapato Zanzibar kuweza kufanya miamala ya malipo ya kodi bila usumbufu wowote kupitia EzyPesa. Hii inamaanisha kwamba walipa kodi wa ndani wataweza kulipa kodi zao husika ikiwamo ushuru wa forodha na kodi zingine kama PAYE na VAT kwenye uingizaji wa biadhaa kupitia mfumo wa EzyPESA.

Akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano hayo Alhamisi ya tarehe 14 Desemba 2017, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Sherif El Barbary akiwa ameambatana na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Amour Hamil Bakari na Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa (Baucha) alisema lengo kuu la huduma hiyo ni kuwawezesha wakazi wa Zanzibar kulipa kodi kwa urahisi zaidi kupitia huduma ya EzyPesa ya Zantel.

Alisema kuwa hatua hiyo ya makubaliano inaendana sawa na dira ya Bodi ya Mapato Zanzibar, yenye lengo la kuwa kitovu cha ukusanyaji mapato chenye ufanisi, jambo ambalo litaiwezesha nchi kuongeza pato la taifa la ndani kwa mwaka (GDP).

“Kama tunaweza kuongeza ukusanyaji wa mapato kupitia huduma ya EzyPesa na pato la Taifa GDP litaongezeka zaidi. Hii itasaidia kuimarisha uchimi wa Taifa zima, na kwa namna nyingine kipato cha mwananchi wa kawaida kitaongezeka.


Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (kulia) na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Ndugu Amour Hamil Bakari (Aliyekaa katikati) wakitia saini ya makubaliano ya kushirikiana katika kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa hivi karibuni mjini Zanzibar. Anayeshuhudia kulia ni Makamu wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Bi. Khadija Shamte Mzee.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (kulia) na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Ndugu Amour Hamil Bakari (Aliyekaa katikati) wakitia saini ya makubaliano ya kushirikiana katika kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa hivi karibuni mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (wa pili kushoto) na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Ndugu Amour Hamil Bakari (wa pili kulia) wakipeana mkono huku wakishuhudiwa na Makamu wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Bi. Khadija Shamte Mzee (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Utendaji wa biashara Zantel, Shinuna Kassim baada ya kutiliana saini ya makubaliano na ushirikiano katika kurahisisha huduma ya ulipaji kodi kwa njia ya simu kupitia huduma ya EzyPesa. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Zanzibar. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...