THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

AGAPE YAKABIDHI BAISKELI KWA VIJANA 15 WALIOHITIMU MAFUNZO YA HISA SHINYANGA

Shirika lisilo la kiserikali la Agape AIDS Control Programme (AACP) limetoa mafunzo ya Hisa kwa vijana 15 kutoka katika kata za Mwamalili,Didia na Masekelo zilizopo katika wilaya ya Shinyanga. 


Pamoja na kuwapatia vyeti vya ushiriki wa mafunzo,shirika la AGAPE pia limekabidhi baiskeli 15 kwa vijana 15 walioshiriki mafunzo hayo ambazo zitawamsaidia kurahisisha kusafiri wanapotoa elimu ya hisa katika jamii. Mafunzo hayo ya uwezeshaji wa vikundi vya hisa ngazi ya jamii yalianza Januari 11,2018 na kufungwa leo Januari 17,2018 katika darasa la AGAPE AIDS Control Programme lililopo katika kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga. Mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo hayo leo,yaliyohudhuriwa pia na maafisa maendeleo kutoka kata hizo tatu,alikuwa Afisa Maendeleo ya Vijana halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 

Meneja Miradi wa Shirika la AGAPE Mustapha Isabuda alisema mafunzo yametolewa ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kuzuia ndoa na mimba za utotoni unaofanywa na shirika hilo kwa kushirikiana na shirika la Firelight. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja
Mgeni rasmi ,Afisa Maendeleo ya Vijana halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya hisa kwa vijana 15 na kutoka kata za Mwamalili,Didia na Masekelo zilizopo katika wilaya ya Shinyanga.Aliwasisitiza vijana kufanya kazi kwa kujituma ili kuleta mabadiliko katika jamii.-Picha zote Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja Miradi wa Shirika la AGAPE Mustapha Isabuda akielezea lengo la mafunzo hayo.Kushoto ni washiriki wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGAPE,John Myola akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.Kushoto ni Kaimu Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,Aisha Mwinshali.Kushoto ni mgeni rasmi ,Afisa Maendeleo ya Vijana halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA